Mchakato wa Yanga kutaka kuboresha timu yao unaendelea na sasa stori kubwa ni wao kutaka saini ya Alphonce Mabula na tayari wameanza mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo huyo mkabaji wa kimataifa wa Tanzania, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya mchakato huo, Yanga inamwona Mabula kama chaguo muhimu la kuongeza ubora, nguvu na ushindani katika eneo la kiungo, na tayari imewasilisha ofa yake kwa lengo la kuhakikisha anasajiliwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, mazungumzo hayo bado hayajafikia mwafaka kutokana na tofauti ya matakwa ya kifedha kati ya pande hizo mbili. Inadaiwa kuwa Msanga anahitaji mshahara wa takribani Dola za Marekani 14,000 (zaidi ya Shilingi milioni 36 za Kitanzania) kwa mwezi, huku Yanga ikiwa tayari kutoa Dola za Marekani 10,000 kwa mwezi.

Mbali na Yanga, kiungo huyo pia anawindwa na klabu mbili za Ligi Kuu nchini Uturuki, Kasımpaşa SK na Gençlerbirliği SK, ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili, jambo linaloongeza ushindani katika mbio za kuwania saini yake.
Kwa kuwa Msanga ni mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu yake ya awali, ana nafasi ya kutathmini ofa zote zilizopo kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wa taaluma yake.

Iwapo Yanga na Msanga watafanikiwa kufikia makubaliano kuhusu maslahi binafsi, usajili huo unatarajiwa kuwa miongoni mwa dili kubwa na zinazovutia zaidi katika dirisha la usajili la msimu wa 2026/27.


