Kuelekea fainali ya kombe la shirikisho Tanzania hapo kesho kati ya mabingwa watetezi Yanga na Singida Black Stars, timu hizo zimekutana na waandishi wa habari na kuongelea kuhusu mchezo huo. Mchezo huo utapigwa kesho kwenye uwanja wa new amani stadium zanzibar majira ya saa mbili na robo usiku.
Kwa upande wa Yanga, kocha Miloud Hamdi akiongea mbele ya waandishi wa habari alisema yanga wamejizatiti kuhakikisha wanachukua kombe hilo kwa ajili ya wananchi ambao wamekuwa wakiwaunga mkono tangu mwanzo wa michuano hiyo mpaka hivi sasa wamefika fainali.
“Kushinda taji kwaajili ya wananchi ni jambo jema sana, tunajivunia hilo kwasababu wamekuwa wakitusapoti katika kila hali hivyo tupo hapa kupigana kwaajili yao, tupo hapa kuwapa furaha, tunayarajia kesho watakuja kwa wingi kwakuwa tunawahitaji sana”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Aliongezea kwa kuwapongeza wapinzani wao kwa kufanikiwa kufika hatua ya fainali na kukiri kwamba wanategemea kukutana na upinzani wa hali ya juu kutokana na ubora wa wapinzani wao kwenye michuano hiyo ambao wamefika fainali kwa kuwatoa vigogo simba sc.
“Kwanza niwapongeze singida black stars kufika fainali, hii siyo kwa bahati mbaya kwasababu wana kikosi kizuri sana. Kwetu sisi Yanga, tunategemea mchezo mzuri na wenye ushindani hapo kesho, tunatarajia kuwa na miongoni mwa mechi bora na ngumu”
“Wachezaji wangu wote wanajua umuhimu wa mchezo wa kesho,wana uzoefu wa kucheza mchezo kama huu, ninatarajia kesho watakuwa wanajeshi bora watakaopambania furaha ya wananchi”
Naye shekhan, akiongea kwa niaba ya wachezaji wa Yanga, ameelezea namna walivyojiandaa na mchezo huo huku wachezaji wakiwa tayari kupambana kuhakikisha wanachukua kombe hilo, lakini pia amewaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi hapo kesho.
“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tupo vizuri na salama, tupo tayari kwaajili ya kuipambania timu yetu, tunawashukuru sana mashabiki wetu kwakutupa hamasa kila wanapotuona, tunawaomba waje kwa wingi hapo kesho ili tufurahi pamoja. Singida ni timu nzuri sana kila mtu anafahamu hili hivyo tunaamini utakuwa mchezo mgumu sana, niwaambie tu wananchi kuwa sisi tupo tayari kwaajili ya kuipambania timu yetu, niwaombe waje kwa wingi”
Vilevile, Singida Black Stars nao walielezea ni kwa namna gani wamejipanga kuweka historia mpya kwenye soka la tanzania kwa kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa kombe hilo. Kocha David ouma alisema
“Tupo na malengo yetu msimu huu na hiyo ndio motisha kubwa sana inayotusaidia tuweze kufanya vizuri kwenye kila mchezo tunaocheza hivyo kesho kutakuwa kuna mchezo mzuri na mgumu wa fainali. Tumejiandaa vizuri”
Na kwa upande wa wachezaji, waliwakilishwa na naodha ayubu lyanga ambaye mbele ya waandishi wa habari alizungumzia malengo waliyojiwekea kama wachezaji kuelekea mchezo huo ambapo alisema “Wachezaji tunajua tunaenda kucheza mchezo wa aina gani. Kwa kuzingatia hayo mwalimu ametuandaa vizuri kwa kila kitu kwenye mchezo wa kesho wa fainali”