BAADA ya maneno kuwa mengi juu ya Yanga kutakiwa kwenda kuweka kambi Morogoro hatimaye uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi mipango yao ya wapi watakwenda kujiadaa na msimu ujao.

Mkurugenzi wa Mashindano Yanga, Thabity Kandoro alisema kocha wa timu Nasreedin Nabi ndiyo mwenye maamuzi ya wapi timu hiyo ikaweke kambi kulinga na mipango ya program yake na hawawezi kuiga watu wanahofanya kwa kuwa haiwasaidii kitu.

 

Yanga ya Kimataifa

Kandoro alisema timu hiyo itaondoka Dar es salaam na kwenda kuweka kambi pale ambapo mwalimu ataona panafaa na kama ataamua kubaki Avic Town bila kwenda pre-season hawatakuwa na kipangamizi kwa kuwa yeye ndiyo bosi.

“Suala la watu Yanga inatakiwa kwenda kufanya maandalizi ya msimu ujao linabaki kuwa jukumu na maamuzi ya kocha Nabi. Yeye ndiyo anajua nini kifanyike kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

 

“Kama ataamua kwenda nje ya nchi timu itakwenda na kama atataka tubakie Dar au nje ya Mkoa yote yanabaki kuwa ni maamuzi yake. Hatuwezi kuwaiga watu fulani kwenda nje wakati mwalimu ameona hakuna tija na kama atahitaji twende Morogoro tutaenda pia,” alisema Kandoro.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa