Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa kupoteza mchezo wao wa kwanza ndani ya uwanja msimu wa 2024/25 ni sehemu ya mpira na wanakwenda kufanyia kazi makosa yaliyopita kwenye mechi zinazofuata.
Yanga baada ya kucheza mechi 8 mfululizo haikupoteza ndani ya ligi mchezo wake wa kwanza kupoteza ilikuwa dhidi ya Azam FC kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 0-1 Azam FC.
Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua wengi walikuwa na hamu kuona klabu inapoteza hivyo wanafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwa imara kwenye mechi zinazofuata.
“Wengi walikuwa na hamu kuona Young Africans inafungwa na imetokea lakini huu ni mpira kwani kila mchezo kuna ushindani mkubwa na ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.
“Wachezaji walijituma mwanzo mwisho na bahati haikuwa upande wetu hatutaki kuamini kwamba tutapoteza mechi zetu zote bado tupo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na tuna mechi za kucheza.”