Yanga Yaibamiza Vibaya Kaizer Chiefs

Klabu ya Yanga wamefanikiwa kuipasua vibaya klabu ya Kaizer Cheifs ya nchini Afrika ya Kusini katika michuano ya Toyota Cup iliyopigwa nchini Afrika Kusini.

Yanga wameichabanga klabu ya Kaizer Chiefs kwa jumla ya mabao manne kwa bila tena wakiwa katika ardhi yao ya nyumbani, Wananchi walionekana kua na kasi kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo na kasi yao iliwanufaisha kwani walifanikiwa kupata mabao mawili ndani ya kipindi cha kwanza.yangaPrince Dube akiwa ndani ya uzi wa klabu ya Yanga anafanikiwa kufunga bao la pili ambapo yeye ndio aliyefunga bao la kwanza katika mchezo wa leo, Huku goli la pili likifungwa na staa wa klabu hiyo Stefane Aziz Ki ambapo kipindi cha kwanza waliondoka wakiwa na mabao mawili mbele .

Kipindi cha pili kiliendelea kwa Wananchi kuendelea na kasi ambayo walianza nayo kipindi cha kwanza ambapo iliwanufaisha ambapo walifanikiwa kupata mabao mengine mawili kupitia kwa Aziz Ki pamoja na Clement Mzize, Hivo kufanya mchezo huo kukamlika kwa ushindi wa mabao manne kwa bila kwa Wananchi.yangaBaada ya kuisambaratisha klabu ya Kaizer Chiefs jioni ya leo klabu ya Yanga sasa akili yao wanaielekeza katika siku ya Mwananchi ambayo itafanyika tarehe 4 mwezi 8 katika dimba la Benjamik Mkapa jijini Dar-es-salaam, Lakini baada ya hapo watakua na kibarua kizito dhidi ya mtani wao klabu ya Simba katika mchezo wa Ngao ya jamii tarehe 8 mwezi wa nane.

Acha ujumbe