Baada ya timu ya Yanga wamepiga hesabu zao wakashtuka viporo viwili vya Simba dhidi ya Namungo vinaweza kuwanufaisha zaidi wekundu hao kwenye mbio za ubingwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amefunguka: “Kwa ratiba hii kama Simba hatakuwa hajacheza mechi yoyote dhidi ya Namungo wakati sisi tukiwa tumemalizana nao maana yake sisi tutakuwa waathirika zaidi katika mbio za ubingwa huko mbele kwa sababu Namungo akishakuwa amecheza na Yanga tena mechi zote mbili lolote linaweza kutokea.”
Yanga vs Simba
“Tumeshawaadikia Bodi ya Ligi waangalie ni namna gani wanaweza kulifanyia hili kazi kabla ya sisi kucheza na Namungo. Simba na Namungo wanatakiwa kucheza hata mechi yao moja halafu mengine ndio yapagwe tukienda hivi kuna uwezekano tukatoa nafasi ya viashirio vya upangaji wa matokeo.”
Yanga vs NamungoIngawa vigogo wa Yanga wanaficha lakini habari za ndani zinaeleza wanaangalia uwezekano wa kususia mechi ya Namungo mpaka Simba icheze nao kwanza.

Habari zinasema Yanga walikuwa wamepanga kuondoka Dar jana lakini wamepiga breki kusikilizia na kama itashindikana watalalamika ngazi za juu.

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

yanga, Yanga Yajipanga Kuisusia Mechi Namungo, Meridianbet

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa