YANGA YAPIGWA MKWARA NA SIMBA

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa ikiwa watani zao wa jadi, Yanga watahama Uwanja wa Azam Complex na kuchagua Uwanja wa KMC, Mwenge basi watakutana na kitu Kizito kutokana na utawala walionao hapo.

YANGA YAPIGWA MKWARA NA SIMBA

 

Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ipo kwenye mpango wa kubadili uwanja wa Azam Complex kwenye mechi zao za nyumbani huku Uwanja wa KMC Mwenge ukitajwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Ally amesema kuwa wao wanatumia uwanja huo kwa mechi za nyumbani wakiwa na uhakika wa kupata matokeo mazuri hivyo wakifuatwa na wengine basi watakutana na balaa zito.

YANGA YAPIGWA MKWARA NA SIMBA

“Naskia Yanga wanataka kuhama Chamazi ikiwa watahamia KMC Complex hapo watakutana na kitu kinachostahili kwa kuwa tumeushika mkononi uwanja ule watapoteana ujue bora waendelee kuwa huko waliko.”

Simba mchezo uliopita ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge wakifikisha pointi 25 nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Acha ujumbe