Yanga Yavutwa Shati na Namungo

Yanga ikiwa Uwanja wa Mkapa imegawana pointi mojamoja na Namungo FC ya Lindi kwenye mchezo wa ligi raundi ya 11.

Bigirimana Blaise, leo Novemba 22 amemwaga machozi baada ya dakika 90 kukamilika kutokana na kitendo cha kukosa penalti dakika ya 90 baada ya kipa namba moja wa Yanga kuiokoa kwa kuitema na aliporudia mara ya pili alipaisha mpira huo mazima.

Yanga ikiwa Uwanja wa Mkapa imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.

Mabao ya timu zote mbili yalipatikana kipindi cha kwanza ambapo Carlos Carlinhos alifunga bao la kwanza kwa Yanga dakika ya 13 kwa pasi ya Kibwana Shomari na dakika ya 16, Stephen Sey alipachika bao la kusawazisha kwa guu la kushoto.

Penalti ya Blaise iliyopaishwa ilipatikana dakika ya 90 baada ya beki,Bakari Mwamnyeto kumchezea faulo kiungo Shiza Kichuya ndani ya 18 na alionyeshwa kadi ya njano.

Mvutano mkubwa ilikuwa ni nani ambaye angepiga penalti hiyo jukumu likawa la Blaise mwenye mabao manne ambaye alikosa penalti hiyo baada ya Mnata kumsoma kwa umakini na kuipangua jumlajumla.

Sare hiyo inaifanya Yanga kugawana pointi mojamoja na Namungo FC Uwanja wa Mkapa huku Mnata akipewa zawadi ya noti na mashabiki baada ya kutimiza majukumu yake kwa umakini.

Yanga inafikisha jumla ya pointi 25 sawa na Azam FC ambayo ipo kileleni kwa idadi ya mabao huku Namungo ikibaki nafasi ya 9 na pointi zake ni 15.


Usichelewe Kukamata Mkwanja Huu!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

 

26 Komentara

    Mechi ilikuwa si ya kitoto

    Jibu

    Yanga hawana jipya hao wamenusurika kidogo tu wangeipata habari yao ila Namongo walijua kunifurahisha jmn

    Jibu

    Hawo yanga hamna kitu ni utopolo tu

    Jibu

    Utopolo kama utopolo

    Jibu

    Kwa jirani zetu wanafurahi kweli jamani kwa mchezo wa Jana yanga waliucheza vilivyo kwenye kiwango bora kwanza walioata nafasi nyingi za kufunga ingawa haikuwa bahati kwao yanga iliyo pita sio ya sasa tukumbuke hasaivi ndiyo tunaionea raha yanga timu ya namungu ilikuwa ni kawaida tu kuifunga yanga lakini hasaivi tunaona inaboreka yaka ila kwa wasio jua mpira wanaongea hatari tunatakiwa kuiangalia yanga iliyopita na hasaivi ndio muongee nyinyi wa porini

    Jibu

    Safi sana namungo maana mashabiki wa yanga mnaongea sana..niliipenda kwakweli ile droo kwenye mechi ya yanga na namungo

    Jibu

    Yanga wamejitahidi

    Jibu

    namungo walijitahidi sana ila yanga walibebwa sana

    Jibu

    Hii mechi ilikuwa yakuvutana mashati vuta nikuvute namongo walikuwa moto Sana isingekuwa ilepenati tungeongea mengine

    Jibu

    Mhii

    Jibu

    Yanga ilibakia kidogo wakalishwe

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Kwa sare hii ni shangwe kwa timu pinzani

    Jibu

    Namungo wanajitahidi sana

    Jibu

    Wamejitahidi sana yanga

    Jibu

    Safi

    Jibu

    🤣🤣🤣

    Jibu

    Habar mbaya kwa mashabik wa yanga ila kwa upande wa pili wanashukuru kwa kupunguzah gape la point na watani wao

    Jibu

    Yanga timu mbovu

    Jibu

    Yanga hawana kaziii

    Jibu

    Namungo jeshi

    Jibu

    Namungo wamejitahid kutoa suluhu a mabingewa

    Jibu

    Bonge la mechi

    Jibu

    😂😂😂

    Jibu

    Nilijua tu watakaa

    Jibu

Acha ujumbe