Patrick Sibomana, mshambuliaji wa Yanga, jana alipindua meza kibabe kwa kufunga bao la kusawazisha mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mchezo huo ulikamilika kwaYanga kufungana na JKT Tanzania, bao 1-1 na kugawana pointi mojamoja, makao makuu ya nchi ya Tanzania, Dodoma. Licha ya Michael Aidan wa JKT Tanzania kufunga bao akiwa nje ya 18 kwa kuachia shuti kali dakika ya 13 halikuwapa pointi tatu JKT Tanzania.
Kuingia kwa Sibomana kulibadilisha mchezo jumla kwa kutuliza timu baada ya kunyanyuliwa benchi na Kocha Mkuu, Luc Eymael dakika ya 52 akichukua nafasi ya kiungo mshambuliaji Mapinduzi Balama.
Bao la Yanga lilipatikana baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima kuachia shuti kali langoni mwa JKT Tanzania lililotemwa na mlinda mlango wa JKT Tanzania ndipo likakutana na guu la Sibomana aliyeujaza moja kwa moja langoni.
Ushindi huo unaifanya Yanga ikusanye jumla ya pointi nne kwa JKT Tanzania msimu huu na mabao manne kwani kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ilishinda mabao 3-2.
Beki Lamine Moro wa Yanga alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 88 kwa kumchezea mchezo usio wa kiuungwana Mwinyi Kazimoto wa JKT Tanzania ambaye naye pia alionyeshwa kadi nyekundu.
Ernest
Hii mechi ilikuwa na vurugu sana walikamiana sana
Povel
Alichokifany beki lamine Moro co fair play kabisa kwn hata FIFA wasisitizah wanamichezo kupendana kwa kitendo kile sheria ifuate mkondo wake iwe funzo kwa wavunja sheria wengne thnks meridian bet tz kwa information
Ester jackson
Mchezo wajana hauku nifurahisha kabisa mana walikuwa wanapigana mitama bila ya kucheza katika nafasi yake
Theonestina
Nilikuwa natamani yanga wafugwe
Neema
Yanga apunguze kujiamini wanawapoteza mashabiki wake
Hamidu
Yanga wazee wavurugu
Leticia
Yanga wapunguze vurugu
Lydia Emmanuel Magoti
Mechi ilikuwa sio poa yanga walishikwa atarii vurugu mtindo moja
Aziza mushi
Yangaa wanacheza kwa fujo Sana
David Pere
Corona imewaathili yanga,lakini kwa upande wa jkt wale ni wajeda muda wote wapo na tizi Kama kawaida
Adelta
Hii mechi ilikuwa na vurugu sana
Salma
Sawa sio mbaya
mwakalosi
hawa utopolo wao ni suluhu tu labda wanaweza kuifunga arsenal tu
Samiah
Yanga hawana lolote vurugu nyingitu
Amani
Simba wapewe ubingwa tu akuna jins# meridianbettz
Theckla
Daaa haikuwa poa
Elika
Yanga ya sasa sio ile yanga ya zamani..yanga wako vibaya sana inatakiwa wafanye na mabadiliko kidogo…kiukweli yanga hawajielewi
Magdalena
Yanga sijui Wana tatzo gani takribani mechi nyingi wanatoka sare wanabidi wabadilike
Caroline
Yanga wanatoa sare sare
Antony Luseno
JKT msimu huu imepania sana vilabu vikongowe asa simba na yanga
Sabrina
Maoni:#meridianbettz asante kwa taarifa
Sadick
Kitendo cha Lamine Moro kimemuondoa kwenye mchezo wa kiungwana na sikuona sababu ambayo ingeweza kumusukuma kufanya vile#meridianbettz
Genia Sikaluzwe
Mmh haikuleta picha nzuri hiyo
Dorophina
Hii mechi kila timu ikiikamia ndio maana kukatokea vurugu nyingi sana
Zeiyana
Yanga bhana wanazidi tu kujishusha hazi wanan,gan,gania msemo wao yanga ya wanachi
Devotha
Haikua mechi nzuri
felister
safi sana yanga
Emmy cleopa
Safi sana yanga
Njiku
Lamine moro hakufanya uungwana na kufanya game iwe na vurugu
warda
Huyu Lamine ameona jina lake halitajwi tajwi ndo kaona atafute kiki#Meridianbettz
Furahav
Yanga hamana kitu.
Gabriel
Yanga ilikuwa inanafas nzur ya ushindi
Hope mwaikuka
Siwaelewag hao
Omary lukumbi
Kusema kwel bwana soka la kibongo linaumiza sana mioyo ya watu mnoo hakuna uhakika wa mechi sisi Tanzania bado sana hasa wanao umia zaid mashabiki wa timu fulan ndio mm binafsi bora niwe uingereza tuu soka la bongo linaumiza sana hisia za watu bora nisiwe mzalendoo tuu wa kuacha.kushabikia nyumban lakn nipate ile burudan nayo itaka
Mwanaidi
Hahaha haya motokeo tuliyategemea kabisa maana wote hawakujipanga
Asia Abdy
Mechi ilikua na vurugu had kero