Zaniolo Kutimkia Aston Villa

Kiungo wa kimataifa wa Italia Nicolo Zaniolo anayekipiga katika klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki anatajwa kuhitajika na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

Zaniolo ambaye alijiunga na klabu ya Galatasaray katika dirisha dogo msimu uliomalizika mwezi Januari akitokea As Roma sasa ameingia kwenye rada tena za vilabu kutoka nchini Uingereza.zanioloKiungo huyo inakumbukwa dili lake la kujiunga na klabu ya Nottingham Forest lilivunjika siku za mwishoni na kusababisha kiungo huyo kutimkia klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki lakini Aston Villa wamerejea tena wakimuhitaji kiungo huyo.

Mkurugenzi wa klabu ya Aston Vila Monchi ndio aliemsajili kiungo huyo kutoka Inter Milan misimu kadhaa nyuma, Hivo inaelezwa kua mkurugenzi huyo ndio anacheza nafasi kubwa kuhakikisha Aston Villa wanampata kiungo huyo.zanioloKiungo Nicolo Zaniolo ameendeleza ubora wake ambao alikua anauonesha ndani ya As Roma akiwa ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa Uturuki pamoja na kufuzu ligi ya mabingwa ulaya.

 

Acha ujumbe