Zanzibar imeruhusu mchezo wa ngumi kufanyika kisiwani hapo, ambapo kupitia hoja iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita aliyoitoa Bungeni.

 

Zanzibar Yaruhusu Ngumi

Kubalika kwa mchezo huo kumekuja baada ya kufanywa kwa utafiti kwa wananchi, na idadai kubwa ya watu kukubaliana kuwa mchezo wa ngumi uruhusiwe huku wachache wakipinga na hivyo basi Serikali nchini humo kuona wauruhusu mchezo huo.

Kwa kundi kubwa sasa nchini humo kukubali mchezo huo, imeonesha Wazanzibar wanauridhia mchezo huo uruhusiwe kisiwani hapo, hayo ameyaeleleza Waziri huyo wa Utamaduni na Michezo Tabia Maulid kwenye taarifa yake ya uanzishwaji wa michezo ya ngumi kwa kamati ya ustawi wa jamii mbele ya baraza.

Hapo mwanzo Zanzibar ilikuwa ikipinga mchezo huo kutokana na madhara yake ambayo yalikuwa yakijionyesha baada ya mtu kupigwa ngumi nzito, wengine kusema pia mchezo huo husababisha matatizo ya ubongo kutokana na ngumi nyingi kutua kichwani.

 

Zanzibar Yaruhusu Ngumi

Vijana wengi walitoa maoni mengi kuwa wanavipaji na huo mchezo, hivyo uruhusiwe visiwani hapo kwani mchezo huo unalipa sana hasa kwa vijana ukizingatia Tanzania kwasasa muamko ni mkubwa. Kwani kuna Mabondia wakubwa akiwemo Hassan Mwakinyo, Ismail Galiatano, Twaha Kiduku, Selemani Kidunda na wengine wengi ambao wameleta ushawishi kwa wengine.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa