Zidane Akataa Kazi Manchester United.

 

Klabu ya Manchester United imemuweka meneja za zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane kipaumbele kuchukua nafasi iliyoachwa na Ole Gunnar Solskjaer lakini meneja huyo ametupilia mbali ombi hilo.

 

Vyanzo mbalimbali vimeripoti Zidane hana mpango wa kuifundisha klabu ya Manchester United, ikumbukwe meneja huyo yupo mapumzikoni tangu mwezi May mwaka huu.

Akiwa Real Madrid, Zidane alifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa UEFA mara tatu mfululizo kabla ya kuondoka na kurejea na kufanikiwa kuchukua La Liga na Spanish Super Cup.

Zidane amekuwa akihusishwa kuifundisha Timu ya Taifa ya Ufaransa na mapema mwaka huu aliweka wazi hamu yake ya kutaka kukinoa kikosi hicho cha Les Bleus.

Ukiachana na Manchester United klabu ya Paris Saint-Germain imekuwa ikimfwatilia mfaransa huyo. Zizzou Bado anatafakari endapo atarejea kufundisha katika klabu au timu ya taifa.

Meneja wa sasa wa Paris Saint-Germain, Mauricio Pochettino amehusishwa na kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer pale Old Trafford.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe