Kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid na gwiji wa timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane amemponza rais wa shirikisho la soka nchini humo Noel Le Graet.

Rais Noel Le Graet aliingia kwenye mzozo mkubwa siku kadhaa zilizopita baada ya kufanya mahojiano na wanahabri na kuongea maneno mabaya juu ya gwiji huyo wa soka la Ufaransa Zidane. Kitendo ambacho kimekera wadau wengi wa soka haswa kutoka nchini Ufaransa ambako gwiji huyo anapewa heshima kubwa.zidaneRais huyo alihojiwa kuhusu gwiji huyo kuomba nafasi ya kuifundisha timu hiyo na Graet kujibu kwa kejeli kua hakupigiwa simu na gwiji huyo na hata ingetokea angepigwa simu basi asingepokea, Baada ya maneno hayo watu mbalimbali akiwemo staa wa klabu ya PSG kylian Mbappe na wazi wa michezo nchini humo walionesha kutokufurahishwa na maneno ya Rais huyo juu ya gwiji huyo.

Baada ya siku kadhaa Rais wa shirikisho hilo Noel Le Graet ameondolewa kwenye wadhifa huo na shirikisho hilohilo nchini humo na hiyo ni kutokana na maneno ambayo alimtolea gwiji Zinedine Zidane. Hivo kuanzia leo Le Graet io Rais wa shirikisho la soka nchini Ufaransa.zidaneNi sahihi sana kusema kua gwiji Zinedine Zidane ndio aliemponza Rais huyo kwani baada tu ya kuzungumza maneno mabaya kwa mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ndipo mambo yalipomuharibikia. Gwiji huyo anapewa heshima kubw nchini humo kwani amefanikiwa kuipa timu hiyo ubingwa wa kombe la dunia mwaka 1998 na taji la mataifa ya ulaya Euro mwaka 2000.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa