Zidane Amsahau Kabisa Mbappe?

Baada ya Zinedine Zidane kurejea tena kama meneja klabuni Real Madrid mwaka Jana, alipania kuboresha zaidi kikosi chake. Zidane alihusishwa na wachezaji kibao katika dirisha la usajili lililofuatia baada ya kurejea.

Mara baada ya kurekea klabuni hapo uhamisho wa Eder Miltao kutoka FC Porto ulithibitishwa kama uhamisho wa kwanza.

Baadhi ya wachezaji waliohusishwa zaidi na kuhamia Real Madrid walikuwa ni Kylian Mbappe na Paul Pogba, japokuwa Zidane alikuwa akisita kuwazungumzia awali alipofika klabuni hapo ila baadaye alifunguka kuwahitaji.

Hata hivyo, nia ya Real Madrid kuinasa sahihi ya Kylian Mbappe bado inaishi wakati akihusishwa zaidi na klabu hii Ukiacha Liverpool wanaotajwa pia kummendea.

Real Madrid wameripotiwa kuwa wapo tayari kwa sasa kuzama mazima kwenye dili la kumsajili Mfaransa Kylian Mbappe anbaye amefunga magoli 90 katika Mechi 120, ikiwa ni jitihada za kuongeza nguvu na kurejesha matumaini ya kikosi cha Zidane.

PSG nao wamejipanga kumbakiza Kylian Mbappe kwa mipango ya kumuongezea mshahara zaidi. Mpappe anaweza kufanaya maamuzi ya kusalia klabuni hapo kwa ili aendelee kulipwa dau nono na kususia dili la Real Madrid na klabu zingine zenye nia ya kuinasa sahihi yake.

Mpaka sasa Mbappe, 21, ana mkataba unaodumu hadi mwaka 2022 na PSG ambao wameshakabidhiwa ubingwa wa Ligue1 baada ya ligi kumalizwa. Na klabu inatajwa kuwa imetoa ofa ya kumpa mkataba mwingine ambao unaweza kumfikisha kwenye mshahara wa £600,000 kama mwenzake Neymar.

Labda Real Madrid wakiwa na mipango ya kumboreshea zaidi mazingira Mbappe, zaidi ya yale ya PSG na kumpa dau nono zaidi basi watafanikiwa kumpata. Zaidi ya hapo, Zidane amsahau staa huyu!

20 Komentara

    we all wonder where he will go, probably join Zidane at Madrid #MeridianBetTZ

    Jibu

    Akimchukua mbape itakuwa poa.

    Jibu

    Madrid wajitahidi wampate kylian mbappe

    Jibu

    Kylian ni mzuri

    Jibu

    Itakuwa vizur wakimpata

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Zidane afanye maamuzi kulingana na mahitaji yake asiingiliwe

    Jibu

    Afanye uamuz sahihi tu

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri ila Ana maitaji nae

    Jibu

    Afanye maamuz magumu tu zidane

    Jibu

    fanya chaguz sahih

    Jibu

    Wakimchukua mbape itakuwa vizuri

    Jibu

    Mbape kiongo mzur uwenda ukimya ukawa na sababu

    Jibu

    Bora alivyorud!! Nyumban ni nyumban tu sasa kila kitu kitaenda sawa

    Jibu

    Zidane ni moja kati ya makocha wenye mafanikio katika mpira na ndo maana naamini katika maamuzi yake ya usajili

    Jibu

    Yeye ndio mwamuzi wa mwisho

    Jibu

    Mbape Yuko vizuri

    Jibu

    Mbape anajua angemsajili ingekua poa

    Jibu

    Kusahaulika hakumfanyi yeye kuwa mchezaji bora

    Jibu

    mbappe anajua

    Jibu

Acha ujumbe