Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane alisema Italia ‘wakati wote imekuwa moyoni mwangu’ na alisisitiza Juventus ‘imekuwa muhimu kwangu kila wakati.”
Kocha huyo Mfaransa alizungumza na Sky Sport Italia baada ya Real Madrid kushinda 3-1 dhidi ya Liverpool Jumanne, wakati Real wakijihakikishia nafuu kuelekea mchezo wa marudiano katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Zidane alifurahi na ushindi lakini alisisitiza wababe hao wa La Liga bado wanapaswa kumaliza kazi hiyo.
Akizungumzia ushindi alisema kuwa licha ya kupata ushindi, wanahitaji kutambua kuwa kuna mechi ya marudiano, na wanahitaji kumaliza kazi waliyoianza.

“Lakini narudia, tunaweza kufurahi na mechi usiku wa leo, kwa sababu tulicheza mchezo kamili.”
Mshindi huyu wa Kombe la Dunia aliulizwa ikiwa inawezekana kumuona akirejea kwenye soka la Italia, na Zidane alisema bado ana uhusiano wa kipekee na Bianconeri, ambapo alikaa miaka mitano kama mchezaji kati ya 1996 na 2001.
“Italia daima iko moyoni mwangu. Juventus daima imekuwa muhimu kwangu, Sijui [kama nitarejea tena Italia]. Sasa niko hapa. Hebu tuone.”
INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.
Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA


warda
Bora aende Italy mana wanamzingua tu
Caroline
Zidane jina kubwa
Sarah
Zidane Yuko vizuri
Hopemwaikuka
Vzur