Zidane Atajwa Man United

Taarifa zinaeleza kua kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane ameingia kwenye orodha ya juu ya makocha wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya kocha Erik Ten Hag ndani ya Man United.

Zidane inaelezwa ni kipaumbele cha mmiliki mpya wa klabu ya Man United Sir Jim Rtacliffe na ndio anaongoza orodha ya kuchukua kibarua cha kocha wasasa ambaye anahudumu ndani ya viunga vya Old Trafford.zidaneHii haitakua mara ya kwanza kwa kocha huyo na gwiji wa zamani wa soka kuhutajika na klabu ya Man United, Kwani alishawahi kuhusishwa pia wakati klabu hiyo imemtimua aliyekua kocha na gwiji wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer.

Muenendo wa kocha wasasa Erik Ten Hag inaelezwa unaacha maswali sana kwa viongozi wa klabu hiyo, Huku wakielezwa kufikria kuachana nae mwishoni mwa msimu huu na kutafuta kocha mwingine ambaye ataweza kurudisha zama bora ndani ya timu hiyo.zidaneKocha huyo wa zamani wa Real Madrid ni moja ya makocha wenye wasifu mkubwa kutokana na alichokifanya ndani ya klabu ya Real Madrid kwa muda mfupi, Hivo Sir Jim Ratcliffe anamuona Zidane kama mtu sahihi wa kuchukua mikoba ya Ten Hag.

Acha ujumbe