Aliyekua kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amezungumzwa kama mtu sahihi wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kwasasa.

Baada ya timu ya taifa ya Ufaransa kutangaza kuendelea na kocha Didier Deschamps mpaka mwaka 2026 ni wazi Kocha Zidane atahitajika kusubiri tena ili apate nafasi ya kuifundisha timu ya taifa lake, Mara nyingi ilielezwa kua gwiji huyo alitazamiwa kuchukua nafasi ya kocha Deschamps lakini imekua tofauti.zidaneGwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Juninho amesema kua kwasasa anaamini kocha sahihi ambaye anaweza kuifundisha timu ya taifa ya Brazil ni Zidane, ambaye kwasasa hana timu ya kufundisha na watu wengi walidhania atachukua mikoba ya Deschamps.

Juninho anasema anaelewa mara nyingi unapotafuta kocha wa timu ya taifa kipaumbele lazima awe mzawa, Lakini kama hakuna mzawa lazima uangalie nje ya nchi yako na ndipo anapoona yeye gwiji Zidane ndio kocha sahihi wa kuinoa Brazil kwasasa.zidaneGwiji Juninho anasema ndani ya Brazil kuna makocha wazuri ikiwemo kocha wa klabu ya Fluminese anaejulikana kama Diniz huku akitajwa kama kocha mzuri nchini humo kama mzawa, Lakini mpaka sasa Diniz hajashinda taji kubwa lolote huku Zinedine Zidane akiwa ni kocha mwenye rekodi kubwa ambapo Juninho anaamini ndio mbadala sahihi wa Tite.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa