Licha ya kuwa kwenye wakati mgumu na kibarua chake kikionekana kuwa mashakani, kocha wa Real Madrid – Zinedine Zidane anasema hanashaka, anasapoti ya klabu.

Klabu ya Real Madrid wameshinda mchezo 1 katika michezo 5 waliyocheza kwa siku za karibuni kwenye michuano yote.

Zilianza kusambaa taarifa kuwa Zidane anamichezo miwili tu ya kuamua hatma yake ndani ya Real Madrid. Mchezo wa kwanza ni dhidi ya Sevilla utakaochezwa leo (Jumamosi).

Zizou amenukuliwa akisema ” Ndio, ninasapotiwa kwa kila kitu na klabu. Siwezi kuridhika tunapopoteza mchezo lakini tunajua wapi tulipo. Tunabahati kubwa ya kuweza kuendelea kupambana na kujitoa kwa hii klabu. Hicho ndicho nitakachokifanya mpaka mwisho wangu.

“Wachezaji wanataka kuendelea kupambania makombe na wamenionesha hilo. Tunafahamu kwa pamoja, tutalishinda hili. Mambo yanapokuwa hayaendi sawa, wao (wachezaji) ndio wanaokuwa wa kwanza kukosa furaha.

“Kwenye nyakati ngumu, tunapaswa kuwa wamoja na kuwa na muelekeo mmoja. Tutayashinda haya.”

Mauricio Pochettino na Raul Gonzalez wanatajwa kama watu wanaowania kuchukua kiti cha Zizou Real Madrid.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Zidane, Zidane “Ninasapoti ya Klabu”, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

  1. Hata kama Zidane atatimuliwa hakuna Kocha mwenye majibu kwa aina ya wachezaji ilionao Madrid kwa sasa. Inakiwa kusajiri world class players na majeruhi wapone ndio muarobaini kuleta ufanisi na kuanza kushinda tena

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa