Hali si shwari ndani ya Real Madrid. Kibarua cha kocha – Zinedine Zidane kipomashakani kwa sasa. Rungu la Bodi ya Madrid litamkosa?

Real Madrid wameshuhudia vipigo viwili mfululizo, dhidi ya Alaves (La Liga) na Borussia Monchengladbach (UEFA). Hii inamuweka Zinedine Zidane katika hali ya sintofahamu kwa sasa.

Madrid ni mabingwa watetezi wa La Liga lakini kiwango cha msimu huu kimekuwa cha kutiashaka kufuatia kuwa na matokeo ya kupanda na kushuka. Kwenye Ligi ya Mabingwa _ UEFA, Madrid wanajulikana ni miamba ya mashindano hayo, msimu huu mambo ni magumu.

Wakiwa katika Kundi B, Real Madrid bado hawajafuzu hatua ya 16 wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja pekee wa kuwapatia au kuwanyima nafasi ya kufikia hatua ya mtoano.

Zinedine Zidane, Zinedine Zidane Tumbo Joto Ndani ya Madrid, Meridianbet
Zidane Akiwa mwenye huzuni baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Shakhtar Donetsk (2-0).

Borussia Monchengladbach na Shakhtar Donetsk zimekuwa mwiba kwa Madrid na Inter Millan kwenye Kundi B. Madrid wanashika nafasi ya 3 na Inter akishika mkia wa kundi hilo. Mchezo wa 6 utaamua nani anasonga mbele, nani anakwenda Europa na nani anaiaga michuano ya Ulaya.

Kwa hali ilivyo, Madrid vs Monchengladbach wanahitaji matokeo ya sare au ushindi kwa Madrid ili Zidane na vijana wake wasongembele. Endapo watatoka sare, timu zote zitafuzu hatua ya 16 bora.

Kama Madrid atapoteza halafu Inter vs Shakhtar Donetsk ikamalizika kwa matokeo ya sare au mmoja wao akashinda, Madrid ataikosa nafasi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa 2020/21.

Hakika hapa ni mchezo wa ‘pata – potea’ kwa Zinedine Zidane na wachezaji wa Real Madrid kwa ujumla.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Zinedine Zidane, Zinedine Zidane Tumbo Joto Ndani ya Madrid, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa