Zirkzee: Nimekuja Uingereza kwasababu ya Man United

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Joshua Zirkzee amesema kilichomvutia kujiunga na klabu hiyo ni klabu yenyewe na sio tamaa yake ya kucheza ligi kuu ya Uingereza kama taarifa mbalimbali zinavyoeleza.

Zirkzee ameyasema hayo akihojiwa chanzo kimoja nchini Uingereza alifunguka”Nini kilinivutia kujiunga na Man United? Kweli… klabu hii ni kubwa sana.”

“Niruhusu niseme kwamba Manchester United ndiyo ilinivutia, siyo Ligi Kuu hasa.”zirkzeeKumekua na maneno kua wachezaji wengi wanavutiwa kucheza ligi ya Uingereza kutokana na ushindani ambao unapatikana katika  ligi hiyo, Lakini imekua tofauti kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi ambaye yeye anasema ukubwa wa klabu ya Man United ndio umepelekea kucheza ligi kuu ya Uingereza.

Mshambuliaji Zirkzee ameanza vizuri ndani ya klabu hiyo ambapo mpaka sasa ameshafanikiwa kufunga bao moja kwenye michezo minne aliyocheza kwenye kikosi hicho cha mashetani wekundu, Huku akionesha kiwango kizuri kwenye michezo hiyo ambayo hakufanikiwa kufunga mabao jambo ambalo limewavutia mashabiki wa klabu hiyo.

Acha ujumbe