Ziyech Miongoni 5 Wataobadilishwa Kwa Ajili Ya Kounde

Timu ya Chelsea imesema ipo mbioni kuwaacha wachezaji watano ili kupata saini ya beki wa kati wa Sevilla Julles Kounde. Miongoni mwa watano hao wanaotegemewa kuachwa ni Hakimi Ziyech.

Ziyech alijiunga na Chelsea majira ua joto mwaka jana kwa dau la Euro millioni 37.5 lakini bado hajaonesha makali yake toka kipindi hicho.

Toka ajiunge na Chelsea amefanikiwa kuhusika na magoli si zidi ya kumi tofauti na matarajio ya wengi. Thamani ya Hakimi katika kikosi cha Chelsea haionekani na pengine Tuchel ameona ni bora amuache nyota huyo wa Morocco.

Ziyech amefanikiwa kuanza katika mechi tano tu kati ya 17 za kocha Thomas Tuchel, hivyo nafasi yake inaonekana kupungua siku hadi siku.

Nyota wengine wanaotegemewa kuachwa kwa mabadilishano ni Kepa Arrizabalaga, Tammy Abraham, Tiemoue Bakayoko and Michy Batshuayi.

Kwa upande wa Kepa, ujio wa Mendy umemfanya awe kipa namba mbili wa Chelsea moja kwa moja. Mendy amekuwa kwenye kiwango bora sana katika mashindano yote aliyecheza akiwa na chelsea msimu huu.

Je, unahisi ni sahihi kwamba Chelsea wanataka huduma ya beki wa kati kwa sasa?


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Watakuwa wamefanya vizuri

    Jibu

    Kweli beki yuko poa wanaacha watu watano

    Jibu

Acha ujumbe