Mark Hughes aliwahi kuichezea Wales na Bayern Munich kwa siku mmoja
Hughes aliposini kama mchezaji wa Bayern alitakuwa kuichezea Wales dhidi ya Czechoslovakia, Prague katika kufuzu Euro ’88. “Nilipata chakula cha usiku na Uli Hoeness aliniuliza ni muda gani mechi Aales inachezwa?” aliniuliza, nikamjibu “ni mchana” akajibu “ Ni sawa, unaweza kucheza mchana na jioni pia.” Hoeness alitazama mechi ya Wales kisha tukapanda ndege hadi Bayern, ilikuwa mechi dhidi ya Borussia Monchengladbach na kipindi cha kwanza kilikuwa kimemalizika. Nilianza kipindi cha pili na Bayern alishinda mechi.

Alvin Martin aliwahi kufunga hat-trick dhidi ya magolikipa watatu tofauti. Beki huyo alifunga magoli hayo wakati West Ham ilipocheza dhidi ya Newcastle mwaka 1986. Goli lake la kwanza alishinda dhidi ya Martin Thomas, ambae ndio alikuwa golikipa, lakini alilazimika kutolewa baada ya kupata. Martin alifunga goli la pili dhidi ya beki Chris Hedworth, ambae nae pia alitolewa kwasababu ya majeraha inamaana aliyefuata ni Peter Beardsley. The Hammers walishinda 8-1.

LászlóKubala ndio mchezaji pekee aliyecheza nchi tatu tofauti (akitambulika na FIFA)
Alizaliwa na wazazi wa Czech wenye asili ya Budapest, Kubala, amekipiga akiwa Barcelona, alichezea Czechoslovakia, Hungary and Hispania.

Jimmy Rimmer ndio mchezaji pekee aliyeshinda medali za Kombe la Ulaya akiwa na vilabu viwili tofauti vya Uingereza. Alikuwa benchi la Man United mwaka 1968 na alianza akiwa Aston Villa 1982 japo alitolewa baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Nigel Spink dhidi ya Bayern Munich.

Zlatan Ibrahimovic amecheza vilabu sita vilivyotwaa Ligi ya Mabingwa lakini yeye hakuwahi kutwaa taji. Straika huyo raia wa Swedeni amechezea Ajax, Barcelona, Inter, Juventus, Man United na sasa AC Milan



Gabriel
Zlata ibramovic Yuko vzur anamikosi
hamidu
wote mafundi wa mpira
Elika
Bado mchezaji mzur
mwakalosi
Man utd tumempa taji la ulaya bhn
Ernest Kimeru
He is the Best but not that lucky.
Rehema Dickson
Ladabra yuko vizuri sema uwezi kubaliwa na kila mtu bahati yake iko mbali 😝
mathayo sonje
tunaweza sema kua hana bahati japo ni fundi wa mpira
Furahav
Fundi mmoja huyo.
isha
bado ni mchezaji mzuri
Neema juma
Hapa siwezi kubagua kwa kweli wote hapa wako biyeeee