Zoma Aipiga Chini Bundesliga

Mohamed Alì Zoma amefanya uamuzi uliowashangaza wengi baada ya kukataa ofa kutoka Bundesliga na kuamua kuendelea kubaki 1. FC Nürnberg, uamuzi ambao sasa unaanza kuzaa matunda makubwa.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 amekuwa mhimili muhimu wa Nürnberg mwanzoni mwa msimu huu, akifunga mabao sita katika michezo sita ya kwanza ya ligi na kuonyesha kiwango kinachozidi kuongeza thamani yake.

Zoma Aipiga Chini Bundesliga

“Haikuwa hali rahisi kwangu mwanzoni, lakini sasa najisikia vizuri sana kuhusu uamuzi wangu. Nina jukumu hapa kwa sababu timu na benchi la ufundi linaniamini,” Zoma alisema.

Nyota huyo alifichua kuwa hakuvutiwa na Bundesliga, ambako Werder Bremen na FC Augsburg zilikuwa zimeonyesha nia kwake. Pia amekuwa akihusishwa na VfB Stuttgart, huku akiwa bado ana mkataba mrefu Nürnberg hadi mwaka 2029.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Uamuzi wa kubaki Ujerumani umeonekana kuwa na faida kubwa kwa klabu hiyo. Zoma, ambaye alizaliwa Italia, amekuwa akionyesha ubora mkubwa mbele ya lango, huku kasi na mguu wake wa kulia vikiwa silaha muhimu kwenye safu ya ushambuliaji.

Zoma Aipiga Chini Bundesliga

Kiwango hicho hakijapita bila kuonekana nchini Italia. Zoma ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia, huku gazeti la Gazzetta dello Sport likimpa nafasi kubwa ya kufanya vyema huko.

Lakini anayefurahia zaidi maendeleo ya Zoma ni kocha wake, Miroslav Klose. Gwiji huyo wa zamani wa Ujerumani na mshindi wa Kombe la Dunia 2014 anaamini Zoma bado hajafichua kila kitu alichonacho. “Laiti angejua kila kitu anachoweza kufanya” Klose alisema, akionyesha wazi kiwango cha imani aliyonayo kwa mshambuliaji huyo.

Klose pia alitania namna Zoma alivyokuja kuvutia macho ya Italia baada ya kuanza kung’ara Nürnberg. “Hawakuwa naye kwenye rada kabisa, halafu ghafla wanaona Nürnberg na kujua nani ni kocha wa hapa,” alisema Klose, ambaye bado ana heshima kubwa nchini Italia kutokana na miaka yake mitano akiwa Lazio.

Zoma Aipiga Chini Bundesliga

Zoma alijiunga na Nürnberg mwaka 2025 akitokea UC Albino Leffe ya Serie C kwa ada ya takribani euro 800,000. Baada ya changamoto za mwanzo, alifunga mabao 14 katika michezo 29 msimu wake wa kwanza.

Nürnberg waliweka bei ya euro milioni 20 kwa ajili ya Zoma majira ya kiangazi, lakini hakuna klabu iliyokuwa tayari kulipa kiasi hicho. Kwa kiwango anachoonyesha sasa, huenda thamani hiyo ikawa mwanzo tu wa safari ya kupanda kwa bei ya mshambuliaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.