Ni takribani miezi 2 imepita tangu Tottenham Hot Spurs imeachana na kocha wake, Jose Mourinho. Tangu kuondoka kwa Mourinho maisha yamebadilika sana klabuni hapo.

Spurs wameshuhudia baadhi ya makocha wakishindwana na uongozi wa Daniel Levy katika kuziba pengo la Mourinho. Pochettino, Sarri, Conte, Fonseca na sasa Gattuso – wote wameshindwa kufikia makubaliano ya kuchukua nafasi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo.

Wakati ambao mashabiki wa Tottenham wanasintofahamu kuhusu hatma ya Harry Kane, bado klabu hiyo inahaha kumpata kocha na kiuhalisia bado hawajaingia kwenye mchakato wa usajili kwani hawana kocha mpaka sasa.

Gattuso

Kupitia umoja wa mashabiki wa klabu hiyo, kulitokea maandamano baada ya kuripotiwa fununu za Gattuso kupewa mikoba ya Mourinho. Mashabiki wa Spurs hawakubaliani kabisa na uwezo wa Gattuso na imeripotiwa kuwa, baada ya mazungumzo kati ya uongozi wa Tottenham na wakala wa kocha huyo – Jorge Mendes, jina la Gattuso limeondolewa kwenye orodha ya makocha wanaoweza kukinoa kikosi hicho.

Sasa itakuaje? Tottenham wataendelea kuzungumka mbuyu katika kutafuta kocha mpya au watachukua uamuzi gani kuelekea msimu ujao?


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa