Ligi Kuu Uingereza imekuwa ngumu kuliko kawaida na jambo ambalo hadi sasa inakuwa vigumu kutathmini ni nani ataweza kupeta kwenye kampeni hiyo ya kutafuta bingwa wa ligi msimu huu au kasi ya Manchester City itaendelea kunyanyasa ndani ya ligi hiyo? Kinachosubiriwa ni suala la muda tu kwa klabu hizo kuendelea kutafuta alama tatu.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute baada ya kila klabu kuwa na kasi ya kutosha kupambana kupata nafasi ya kushinda ili kujizolea alama ndani ya mchezo huo. Ndani ya pambano hilo City alikuwa na kila sababu ya kushinda lakini mambo yalienda nje ya malengo ambapo ilishuhudiwa wakimaliza mechi hiyo bila kuamini kilichotokea.

Wengi wakaanza kuamini kwamba ule mzimu wa Jesus umezidi kuendelea ndani ya ligi pia baada ya kukutana na jambo hilo hata ndani ya timu ya taifa. City walipata goli dakika za lala salama kabisa lakini maamuzi ya VAR yaliamua kwamba goli lile lilikuwa na walakini na kuamua kwamba lifutwe.

Teknolojia hiyo imeingia ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwa msimu huu hivyo aina ya maamuzi ambayo yalitolewa kwa upande fulani yaliwaathiri sana wenyeji hao ambao walikuwa wameshangilia kuashiria wamefanikiwa kupata alama ndani ya mechi hiyo. Lakini hali ilibadilika ghafla baada ya kuangalia kilichotokea awali.

Matokeo hayo yalionekana kuwaangusha sana City na hata kuwapoteza baadhi ya wachezaji kuanza kupandisha hasira zao kwa muamuzi wa mchezo huo. Goli lililofungwa lilikuwa sahihi kabisa lakini kilicholeta utata ni kwamba goli hilo lilifungwa mara baada ya mpira kugusa mkono wa mchezaji kwenye harakati za kugombania mpira.

Sakata la matokeo hayo mbali na kuwa ni mapema sana mwa ligi lakini ni kipimo cha kujua kuwa nini kinaweza kutokea kwa hapo baadaye. Kawaida ya City katika michezo yake huwa ni kutafuta alama za mapema sana ili waweze kuwa na faida ya hapo baadaye ikitokea wenzake wanaanza kulegalega.

Pochettino ameridhika na matokeo ambayo yametokea ndani ya mechi hiyo na kusema yote yaliyotokea ni masuala ya kiteknolojia na hayawezi kuzuilika kwa hali hiyo. Na anaona kwamba amefurahishwa na kiwango cha timu yake kwamba wanaonekana kubadilika kutokana na mfumo wa timu pinzani.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa