Winga wa Man City na timu ya Taifa ya Uingereza – Rahim Sterling, anatarajia kufanya mazungumzo ya hatma yake na uongozi wa klabu hiyo.

Sterling ambaye kwa sasa anaitumikia Timu ya Taifa, anaripotiwa kukaa kikaangoni na uongozi wa klabu hiyo ili kujua hatma yake ni nini wakati huu ambao amebakiza miaka 2 kwenye mkataba wake na timu hiyo.

City imeshaachana na baadhi ya wachezaji nyota ambao waliwahi kucheza na Rahim katika muda wa miaka 10 iliyopita ambayo kwa hakika ni muda ambao City wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni sambamba na kutwaa makombe 4 ya EPL na kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

Sterling, Sterling Kukaa Kikaangoni na Man City., Meridianbet
Spurs hawatopokea ofa yeyote yenye thamani ya chini ya pauni milioni 150 ili kumuachia Harry Kane.

Swali ni Je, Rahim ataachiwa kuondoka klabuni hapo kama ilivyokuwa kwa Aguero, Kompany, Toure, Fernandinho na David Silva au atatumika kama sehemu ya usajili wa wachezaji wengine.

City wanahusishwa na usajili wa Harry Kane na Jack Grealish na endapo watafanikiwa kuwasajili wachezaji hao, ni dhahiri kuwa baadhi ya wachezaji wa City watauzwa. Kwa upande wa Sterling, ameweka wazi kuwa hataki kuwa sehemu ya usajili wowote na kwamba hatma yake haitoamliwa na mtu mwingine yeyote zaidi yake.

Tamko la Rahim linakuja wakati ambao alihusishwa na Spurs kama sehemu ya mchakato wa kumsajili Kane kwenye dirisha hili la usajili.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa