Wakati wa sakata kubwa la EUROPEAN SUPER LEAGUE, Kuna Shabiki wa Chelsea alinyanyua bango lilisomeka “Bring back our cold nights in Stoke”.

stoke

Watu wengi wanajiuliza Kwanini Stoke City inatajwa sana? Kwanini Hashtag ya Monday Night Football in Stoke inatamba sana? Hii ndio klabu na Britannia ndio dimba lililokuwa linaamua mabingwa wa EPL bwana!

Cesc Fabregas mtoto kutoka Hispania, wakati wachezaji wanatoka vyumbani kuelekea kupasha misuli moto kabla ya pambano lao dhidi ya Stoke 2006, akamuuliza Reyes, hivi huo uwanja upo wapi?? Reyes alicheka na kumwambia uwanja upo chini ya hilo barafu.

stoke, Stoke City na Go Hard or Go Home, Meridianbet

Wachezaji walikuwa wanawaza kucheza kwenye usiku mzito na wa baridi kali, nyuzi joto ikianguka mpaka -5, ukungu na hamuonani ila wenyewe wanasema, a normal Saturday afternoon in Stoke.

Mtoto bishoo wa Kireno, Cristiano Ronaldo aligusa mpira mara ya kwanza akajikuta chini juu ya barafu, aligusa mpira mara ya pili akajikuta tena chini, alipotaka kuanza kulalama akasikia Jonathan Walters akimwambia, GO HARD OR GO HOME, yani ukitaka pambana au ukitaka amsha nenda kwenu.

stoke, Stoke City na Go Hard or Go Home, Meridianbet

Watu wengi mnasema Mashabiki wa Liverpool ni wahuni na Watukutu, watu wengi mnawapa sifa nyingi Liverpool ila niwakumbushe 1990 wakati huo Liverpool ipo chini ya Graeme Souness, Stoke City waliamsha vibe, wakiimba Anthem yao maarufu inaitwa Delilah.

Souness alishtushwa na ile kelele, ikalazimika kumwita Msaidizi wake mmoja, kwakuwa kila akitoa maagizo hasikiki vyema, tena ndani ya Anfield, Stoke City waliamsha kiasi ambacho watu hawasikilizani uwanjani.

stoke, Stoke City na Go Hard or Go Home, Meridianbet
Souness

Sababu kubwa kuzuiwa kutumia Nyimbo zao zingine ilikuwa kutokana na beti zao kuwa na maneno ya viapo vikali, “Nitailinda Stoke, kwa gharama ya uhai wangu”, “Nitakufa Mimi na wewe kwa ajili ya Stoke” ndio hapo Police walikataza.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

stoke, Stoke City na Go Hard or Go Home, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa