Baada ya bao muhimu la Suarez pale Madrid, Atletico ilitangazwa bingwa wa Laliga toka ifanyike hivyo mwaka 2014. Suarez alidondosha chozi baada ya kuwa chachu kuu ya ushindi wa mechi hiyo.

Suarez amekuwa chachu ya mafanikio ya Atletico Madrid baada tu ya kusajiliwa kwa dau la dola milioni 7 tu akitokea Barcelona. Amemaliza msimu huu pale Atletico akifunga magoli 21, huku 17 kati ya hayo yakisaidia timu yake kukusanya alama 35.

Akionesha kufurahia na kuishukuru Atletico kwa kumuamini kipindi ambacho Barcelona haikuona thamani yake. Kitendo cha Luis kuuzwa kilionekana kuwakasirisha wachezaji na wadau mbalimbali wa Barcelona, akiwemo Lionel Messi. suarez

Baada ya mechi hiyo dhidi ya Valladolid, ambako Luis alifunga goli la pili na kufanya ubao wa matokeo kuonesha 2-1, baada ya kuwa nyuma kwa goli moja mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza. Suarez aliangusha chozi na kulia kwa furaha kwa kufanya makubwa katika michuano hiyo ya Laliga, ambayo ilikuwa ya vuta ni kuvute msimu huu.

Yaliyosemwa, “Barca haikuniona thamani yangu, lakini Atletico Madrid ikanifungulia milango. Nitaishukuru klabu hii daima kwa kuniamini”, alisema Luis.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa