Klabu ya soka ya Watford wameshindwa kuvumilia matokea ambayo klabu hiyo imekuwa ikiyapata ndani ya ligi hiyo kwa kuangalia mbadala wa kipi waweze kukifanya ili kusuka mipango ya kimafanikio upya kikosini hapo. Maamuzi yaliyochukuliwa na bodi hiyo ni kumfuta kazi kocha wa klabu hiyo Sanchez ili kujipanga upya zaidi na kuona namna ya kuifanya timu hiyo isonge mbele zaidi.

Klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania, Simba imepishana njia na kocha wao aliyeleta mafanikio na kuipa jina zaidi klabu hiyo kwa kuirudisha kwenye ramani, Patrick Aussems. Maamuzi yaliyotolewa ni kumfuta kazi kocha huyo kutokana na kinachodaiwa kuonesha utovu wa nidhamu kwa kuitelekeza timu na kuamua kuondoka klabuni hapo. Kocha huyo aliondoka bila taarifa zozote zile klabuni hapo na hata alipopewa nafasi ya kutolea maelezo juu ya uwepo wake alishindwa kuweka bayana nini kimetokea. Pia, bodi ya klabu inadai mbali na kumvumilia kocha huyo kwa kushindwa kufikia malengo ya klabu msimu huu lakini hajaonesha ushirikiano zaidi ya kuanza kugawa wachezaji.

Klabu ya Real Madrid ipo mbioni kushawishi uongozi wa klabu ya Manchester United kuwauzia nyota wa klabu yao, Paul Pogba ambaye walimuweka kwenye malengo yao tangu mapema msimu uliopita japo malengo yao hayakukamilika. Nia ya klabu hiyo bado haijapotea hadi sasa. Kama sehemu ya biashara wanafikiria kutoa kitita cha zaidi ya £72m na wachezaji wawili ambao ni James Rodriguez na Mariano. Kinachosubiriwa ni utayari wa klabu hiyo kukubali ofa hiyo kwa kipindi hiki ili waweze kuifanya biashara hiyo ambayo Madrid wanaamini ina faida kubwa sana kwa upande wao.

Klabu ya Rennes inatambua kwamba nyota wao wa miaka 17, Eduardo Camavinga anaviziwa na klabu kubwa za soka kutokana na uwezo wake anaouonesha klabuni hapo. Barcelona na Manchester United ni klabu ambazo zinaonesha nia ya kumsajili nyota huyo hivyo na wao kama klabu wameweza kuweka dau la £52m kama kiwango cha kumuuzia nyota huyo.

Leicester wameweka kizuizi fulani baada ya kufurahishwa na uwezo unaooneshwa na kocha wao wa sasa, Brendan Rodgers juu ya kushika nafasi yake kwa kuweka kifungu fulani ambacho klabu yoyote itakayomhitaji mwalimu huyo italazimika kulipa kiwango cha £14m ili kumnasa. Kipande hicho ni ulinzi tosha kwa Leicester.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa