Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves, baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wao.
Taarifa hiyo iliyotolewa Mei 06, 2026 na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa umefikia uamuzi wa kumfuta kazi kocha huyo huku ukimshukuru kwa mchango wake mkubwa ndani ya timu katika kipindi chake cha kuinoa Yanga.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya kuondoka kwake, Pedro Gonçalves anaiacha Yanga ikiwa kwenye kiwango bora ndani ya ligi. Takwimu zinaonyesha kuwa ameiongoza timu hiyo katika michezo 19, akipata ushindi 14, sare tano na hajapoteza mchezo wowote. Katika kipindi hicho, Yanga imefunga mabao 44 na kuruhusu mabao matano pekee huku ikipeperusha bendera ya kuongoza ligi katika nafasi ya kwanza.
Katika taarifa hiyo, viongozi wa Yanga wamemtakia kila la heri Pedro Gonçalves katika majukumu yake yajayo, wakisisitiza kuwa mchango wake utaendelea kuthaminiwa ndani ya klabu hiyo yenye historia kubwa Tanzania.
Kwa sasa kikosi hicho kitaendelea chini ya makocha Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi ambao wataiongoza timu hadi mwisho wa msimu huku mashabiki wakisubiri kuona hatma ya benchi la ufundi la mabingwa hao wa Tanzania.


