Katika hali halisi ni vigumu sana mtu kushika nafasi ya mtu mwingine na kufanya kiuhalisia kama yule mtu alivyokuwa anafanya kitu hicho. Katika soka pia ipo hivyo si rahisi kupata mchezaji anayeweza kufanya kama yanayofanywa na mwingine kwani kila mmoja ana nafasi yake na ana aina yake ya uchezaji na kujituma ili kuwa katika kiwango cha juu na kile kinacho ridhisha zaidi ya mwingine.

Kinapofika kipindi cha usajili mashabiki wengi huwa na wasiwasi sana juu ya wachezaji wanaowaamini kama ikitokea wakapata ushawishi wa kifedha au wakitaka kubadili maisha yao kwa kwenda kupambana katika klabu nyingine; haya ni baadhi ya mambo ambayo mashabiki wengi huhofia sana.

Baadhi ya vitu mashabiki wa Chelsea wasingependa kuviona kwao ni suala la kuondoka kwa kiungo wao mahiri na mwenye uwezo wa pekee; Kante ambaye amekuwa mhimili mkubwa sana kwao kwa sasa katika kikosi hicho. Kante ni aina ya wachezaji ambao klabu yoyote ile ingependa kuwa nao. Leo unaletewa baadhi ya wachezaji ambao kwa kiwango fulani wanaweza kuwa mbadala wa mchezaji huyo, endapo akiamua kuanza maisha nje na pale.

Sergej Milinkovic-Savic

Raia huyu wa Serbia na mchezaji wa Lazio sio tu ni aina ya wachezaji wanaoendana na Kante kiuchezaji, bali ni mtu mwenye uwezo wa hali ya juu katika kucheza na kutawala eneo zima la kiungo ambayo ni kazi pekee kiungo anapaswa kuifanya uwanjani ili kuendana na kasi ya mechi na aina mpira unavochezwa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anahusishwa na kuwafanya hata klabu kubwa kumtolea sana macho kutokana na uwezo wake wakiwemo Chelsea na Madrid maana kwa namna anavyocheza ni suala ambalo linawasaidia wao kuendana na mifumo mbalimbali ndani ya klabu zao.

Jean Michael Seri

Wanaofuatilia soka duniani kote hawawezi kuwa na wasiwasi kwa uwezo unaooneshwa na raia huyo wa Ivory Cost kwa sasa. Hadi imefikia akapewa jina la ‘Xavi wa Kiafrika’. Hiyo imetokana na uchezaji wake unaovutia tangu ajiunge na Nice. Ameisaidia sana klabu hiyo kusonga mbele kwenye ligi hiyo kutokana na kasi yake na nidhamu mchezoni. Endapo Kante ataamua kuonesha dalili zake za kuondoka ni wazi kabisa kwamba nguvu zote za kipesa na ushawishi zinaweza kuelekezwa kwake ili kuweza kurudisha nguvu kikosini kwao.

Arturo Vidal

Kiungo mtukutu mwenye nguvu, stamina na hata akili ya mpira amekuwa nguzo toka alipokuwa Bayern na bado anaonesha makucha yake hata ndani ya klabu yake mpya ya Barcelona. Nia aina ya wachezaji ambao wakilishika dimba wanaufanyia mpira vile wanavyotaka wao. Hakika naye angeweza kuishika mikoba hiyo vizuri sana.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa