Baada ya familia ya Glazer kumiliki klabu ya Man United tangia mwaka 2005, wamekuwa wakipokea ofa kadhaa bila kufanya maamuzi magumu.

Hata hivyo, kila jambo linawezekana! Mambo yanaweza kubadiliika na tukashuhudia mabadiliko ya wamiliki wa klabu hii kongwe wakati ikiwa inaendelea kupambana kurejesha hadhi yake.

Stori kubwa wakati Man United wakiendelea kupambana kurejesha heshima yao EPL ni kuwa Mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Prince Mohammed Bin Salman ametoa ofa ya kuinunua klabu ya Man United.

Jarida la The Mirror, linamtaja Prince Mohammed Bin Salman kuwa yupo tayari kufanya ununuzi wa klabu hiyo wakati familia ya Glazer wakiwa wamemiliki klabu hiyo kwa miala 14.

Hata hivyo, wakati Prince Mohammed Bin Salman akihitaji kuwekeza kwenye klabu ya United. Familia ya Glazer pia inatajwa kuwa haipo katika mpango wa kuiuza klabu hii. Hii inaweza kuwa kikwazo kwa kutimia kwa nia ya mwana wa mfalme kumiliki klabu ya United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa