Tetesi zinasema Liverpool wana nia ya kumsajili tena mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Luis Suarez, mwenye umri wa miaka 34.

Mshambuliaji wa safu ya kati wa Atletico Madrid Mhispania Diego Costa, 32, ataichezea Benfica msimu ujao baada ya kuafikia makubaliano na klabu hiyo ya Ureno.

Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon hana uhakika kama klabu hiyo ina pesa za kusaini mkataba na mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, msimu huu.

Tetesi zinasema Real wanataka kumrejesha mshambuliaji Mhispania Brahim Diaz, 21, kikosini kufuatia kukamilika kwa mkataba wake wa mkopo katika AC Milan.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema mchezaji wa Villarreal Mhispania Paul Torres mwenye umri wa miaka 24, anataka kuhamia katika klabu ya Manchester United msimu huu .

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Alan Hutton ameitaka klabu hiyo kusaini mkataba na mlinda mlango wa England Sam Johnstone kutoka West Brom ili azibe pengo la Hugo Lloris.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright anasema klabu hiyo inapaswa kusaini mkataba wa kudumu na kiungo wa kati raia wa Norway Martin Odegaard, 22, kutoka Real Madrid msimu huu.

Sunderland wameanza mazungumzo na Wolves kwaajili ya kusaini mkataba na mlinzi Muingereza Dion Sanderson, 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkataba wa deni kwa pauni milioni 2.

 

Tuchel: Namuani Pulisic Lakini Itabidi Asubiri

Tetesi zinasema Barcelona inataka kumuuza Griezmann na kiungo wa kati Mbrazili Philippe Coutinho, 28.

Winga wa Chelsea Christian Pulisic, 22, anasema anataka kuiwakilisha Marekani katika michezo ya msimu huu ya Olympiki iliyopangwa upya mjini Tokyo.

Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Marco van Basten, 56, anasema sheria ya kuotea ( offside) inapaswa kuondolewa.

Tetesi zinasema Uefa inajiandaa kuondoa sheria za Kifedha za Fair Play ili kuruhusu udhibiti mzuri zaidi wa fedha zao.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa