Tetesi zinasema Lionel Messi, 33 yuko tayari kusaini mkataba mpya Barcelona kufuatia uchaguzi wa rais mpya Joan Laporta.

Tetesi zinasema Real Madrid hawapo tayari kumuachia Martin Odegaard kujiung ana Arsenal kwa mkataba wa kudumu, kwani yupo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo.

Kiungo wa kati wa Liverpool Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, atahitaji kusubiri hadi Barcelona watakapomuachilia mchezaji wa kati Mbosnia Miralem Pjanic, 30, kabla hajakamilisha mkataba wake wa kuhamia Nou Camp.

 

Wijnaldum

Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Inter Milan na Ubelgiji Romelu Lukaku, 27, pia analengwa na meneja wa klabu ya Barcelona Ronald Koeman.

Tetesi zinasema Liverpool wanaangalia uwezekano wakumsajili mchezaji wa PSV Eindhoven Donyell Malen, 22 licha ya kuhusishwa na Juventus na AC Milan.

Tetesi zinasema Meneja Ole Gunnar Solskjaer, 48, anatarajiwa kupata mkataba mpya hata kama Manchester United watamaliza msimu bila kushinda kombe lolote.

Mmiliki wa klabu ya Sheffield United Prince Abdullah anasema hakutaka kumfukuza Chris Wilder na anadai meneja huyo wa zamani wa Blades aliomba malipo ya pauni milioni 4 ajiuzulu.

Tetesi zinasema mshambuliaji wa Nigeria Kelechi Iheanacho, 24, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Leicester City msimu huu.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Mchezaji mkongwe wa Roma Francesco Totti, 44 anaweza sasa kufanya kazi kama wakala wa michezo baada ya kukamilisha taratibu za kujiuzulu kwake nchini Italia.

Tetesi zinasema Barcelona wanamtaka mchezaji wa safu ya mashambulizi ya Eintracht Frankfurt Mreno Andre Silva.

Hali ya baadaye ya Mkufunzi Zinedine Zidane katika Real Madrid baada ya msimu uliosalia imesalia kutojulikana, huku Shirikisho la soka la Ufaransa likionyesha kumtaka . Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 48-bado ana mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2022.

Egypt wametangaa kuwa wanamtaka Mohamed Salah kuunda sehemu ya kikosi chao cha mwisho kwa ajili ya michezo ya olympiki, hii ikimaanisha kuwa atakosa mechi za awali za maamndalizi ya msimu wa soka katika Liverpool.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina, Guido Rodriguez, 26 anasema anatambua kuhusu taarifa zilizoripotiwa kuwa Arsenal wanamuwania.

Liverpool wameonyesha nia yao kumsajli mchezaji wa safu ya mbele Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, ambaye alikaribia kujiunga na Reds mwaka. Hatahivyo, Inter Milan na Rennes pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa