Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 29, ameingia makubaliano ya awali kubaki Paris St-Germain mpaka mwaka 2026 na sasa klabu hiyo ya Ufaransa inafanya jitihada ya kufanya makubaliano kama hayo na mshambuliaji wa Kifaransa Kylian Mbappe,22.

Tetesi zinasema wakala Mino Railola anahitaji pauni milioni 20 kama kamisheni katika dili la usajili wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Erling Haaland.

Haaland, 20, amekuwa akihusishwa na taaarifa za kuhamia Barcelona lakini kocha Ronald Koeman amesema uamuzi wowote kuhusu uhamisho lazima ufanywe na rais Joan Laporta.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema Lionel Messi anasubiri kuona ombi la Laporta kwa ajili ya mustakabali wa Barcelona kabla ya kuamua kusalia kwenye klabu hiyo au kujiunga na PSG au Manchester City.

Angel di Maria amesema angependa kucheza sambamba na Messi kwenye kikosi cha PSG ikiwa mshambuliaji huyo, 33 ataondoka Barcelona.

Tetesi zinasema kocha wa Leicester Brendan Rodgers ana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati Mskoti Callum McGregor,27, kutoka klabu ya Celtic.

Kocha wa West Ham David Moyes amesema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya wachezaji Declan Rice,22, na kiungo wa kati wa Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, 26 msimu huu wa joto.

Manchester United na Juventus ni vilabu vinavyoonesha nia zaidi ya kumnasa mshambuliaji wa Barcelona, Mfaransa Ousmane Dembele,23, lakini Liverpool na PSG nao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amemuondoa beki wa kati Antonio Rudiger,23 mazoezini siku ya Jumapili baada ya kuzozana na mlinda mlango Kepa Arrizabalaga,26, baada ya kufungwa 5-2 na West Brom Jumamosi.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Winga wa Uhispania Lucas Vazquez,29, ambaye mkataba wake na Real Madrid unakwisha mwishoni mwa msimu, atapatiwa mikataba na Manchester United, Chelsea, AC Milan na Bayern Munich.

Tetesi zinasema Juventus hawana uwezekano wa kulipa pauni milioni 8.5 zaidi kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwa mwaka mmoja mwingine kwasababu ya changamoto za kifedha.

Beki wa kati wa Everton na Colombia Yerry Mina,26, anataka kuhamia ligi ya Serie A msimu huu wa joto, huku Inter Milan na Fiorentina nao wakimtolea macho mchezaji huyo.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa