Tetesi zinasema Aguero yuko tayari kukosa ligi ya mabingwa msimu ujao ili asalie ligi ya primia huku Chelsea na Tottenham zikiwa miongoni mwa vilabu atakavyovifikiria.

Manchester United inaweza kujiunga na Liverpool katika mbio za kupata saini ya mlinzi wa kati wa RB Leipzig Ibrahima Konate. Mchezaji huyo,21 anatarajiwa kugharimu kiasi cha takribani pauni milioni 34.

Tetesi zinasema West Ham itajaribu kumsajili kiungo wa kati Jesse Lingard kwa mkataba wa kudumu msimu huu, lakini wanahofia Manchester United watataka dau la juu kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 28.

 

West Ham United

Arsenal itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Kifaransa Alexandre Lacazette katika dirisha la usajili katika majira ya joto. Inter Milan, Roma, Sevilla na Atletico Madrid zinataka kumnyakua mchezaji huyo mwenye miaka 29.

Tetesi zinasema Tottenham wanajiandaa na uhamisho wa kiungo wa kati wa RB Leipzig Marcel Sabitzer, 27.

Tetesi zinasema Juventus, Arsenal na Chelsea wanamtolea macho kiungo wa kati wa AC Milan, Mturuki Hakan Calhanoglu, 27, ambaye anaweza kupatikana kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu.

Mshambuliaji wa Villarreal Gerard Moreno, 28 ni miongoni mwa wachezaji muhimu msimu huu-hata hivyo gharama ya uhamisho ya Mhispania huyo ni pauni milioni 85.6.

Tetesi zinasema mshambuliaji Theo Walcott,32, atajiunga na Southmpton kwa mkataba wa kudumu , mara mkataba wake wa kucheza kwa mkopo Everton utakapokwisha.

Tetesi zinasema Everton itahitaji kiasi cha pauni milioni 21.4 ikiwa watamuuza mlinzi wa kati Yerry Mina.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amemtaka mshambuliaji Ousmane Dembele,23 kusalia kwenye klabu hiyo, ingawa Manchester United imeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.

Tetesi zinasema Manchester City inamtolea macho kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge,23 wakati wakitafuta mbadala wa kiungo wa Brazil Fernandinho,35.

Baba wa kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ameitaka Arsenal kumruhusu mchezaji huyo, 25, anayecheza kwa mkopo Atletico Madrid, kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa