Tetesi zinasema Arsenal imerejesha nia yao tena kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 28.

Manchester City wanalenga kukubaliana kuingia mkataba mpya na washambuliaji wa England Phil Foden,20, na Raheem Sterling, 26 kabla ya mwishoni mwa msimu baada ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne,29, kuongeza mkataba wake wa mpaka mwaka 2025.

Tetesi zinasema Manchester City haitamfuatilia mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi mpaka mchezaji huyo, 33, atakapoweka wazi kuwa anataka kuondoka Barcelona.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Chelsea wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 86.3 kwa ajili ya mshambuliaji Mbelgiji anayecheza katika klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku, 27, endapo the Blues watashindwa kumsajili mshambuliaji Erling Braut Haaland,20, wa Borussia Dortmund.

Tetesi zinasema Tottenham watajaribu kumsajili mlinzi wa kati wa Southampton Jannik Vestergaard, 28, mwenya thamani ya pauni milioni 18, baada ya dirisha la usajili kufunguliwa.

Tetesi zinasema Liverpool wameiambia RB Leipzig kuwa hawatamsajili mlinzi wa kati, Mfaransa Ibrahima Konate,21,

Reds watakabiliwa na ushindani wa Chelsea katika kumnasa kiungo wa kati wa Ajax Ryan Gravenberch,18, ambaye anatazamwa kuwa mbadala wa Georginio Wijnaldum,30.

Tetesi zinasema kocha wa zamani wa Bournemouth anamtaka mshambuliaji wa Everton Josh King,29, kuwa mchezaji wa kwanza kumsajili akiwa kocha wa Celtic.

Tetesi zinasema Barcelona wanataka kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Kifaransa Ousmane Dembele mpaka mwaka 2025, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2022.

Barcelona wameendelea kumfuatilia mlinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia lakini wametoa ofa pungufu ikilinganishwa na iliyowekwa mezani mwaka jana uliopita.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

 

Bayern Munich imethibitisha kuwa mlinzi wa Kijerumani Jerome Boateng, 32, ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu.

Southampton na West Ham ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na kiungo wa kati wa Manchester City Yangel Herrera, 23, ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Granada.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka Lucas Torreira kuwa na subira baada ya kiungo wa kati wa Uruguay, 25, ambaye anacheza kwa mkopo Atletico Madrid, kuomba kuachana na washika bunduki hao kwenda Boca Juniors.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa