Tetesi zinasema, Jose Mourihno aliyetimuliwa kazi na Tottenham mapema wiki iliyopita amejitosa kugombania nafasi ya kuifundisha klabu ya Celtic.

Valencia pia wamehusishwa na kocha huyo wa Ureno, wakati mmiliki wa klabu hiyo Peter Lim anajiandaa kumtimua kocha wa sasa Javi Gracia kumleta Mourinho aliye na emri wa miaka 58.

Tetesi zinasema, Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers, 48, amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Tottenham.

 

Brendan Rodgers

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anahofia huenda hadi wachezaji 10 wangeondoka klabu hiyo msimu huu wa joto kama asingemuondoa Mourinho. Levy alikuwa na wasiwasi zaidi kuhusu hatma ya Harry Kane, 27, na Dele Alli, 25, pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 31, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Real Madrid.

Barcelona wamempatia ofa ya mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 32. Muargentina huyo yuko huru kuondoka kwa uhamisho wa bure mkataba wake utakapomalizika uwanja wa Etihad msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema, Real Betis wanataka kumsajili mlinzi wa Ivory Coast Eric Bailly,27, kutoka Manchester United msimu huu.

Aston Villa huenda wakamnunua kiungo wa kati mshambulizi wa Manchester United na England Jesse Lingard msimu huu wa joto. West Ham United pia wanapania kumpatia mkataba wa kudumu Lingard mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa akiwachezea kwa mkopo tangu mwezi Januari.

Tetesi zinasema, beki wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car, 24, ana matumaini Liverpool itafufua azma ya kumtaka ajiunge nao hasa wakati huu ambapo klabu yake iko tayari kumuachilia.

 

West Ham United

West Bromwich Albion wamejitolea kusalia na kipa wao Sam Johnstone,28, katika uga wa Hawthorns. Manchester United na West Ham pia wanamtaka mchezaji huyo raia wa Uingereza.

Tetesi zinasema Newcastle United wanamtaka beki wa Benfica wa chini ya miaka 21- Mreno Nuno Tavares.

Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Brighton & Hove Albion kuhusu mpango wa kumpatia mkataba wa kudumu kipa wa Australia Mat Ryan,29, ambaye kwa sasa yuko klabu hiyo kwa mkopo.

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, ameanza mkakati wa kuhamia Madrid. Mshambulizi huyo wa Ufaransa bado hajakubali kutia saini mkataba mpya PSG na kwa muda mrefu amehusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa