Tetesi zinasema Rais wa Barcelona Joan Laporta anashughulikia mkataba wa miaka mitatu kumpa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi katika jaribio la kumshawishi mchezaji huyo wa miaka 33 abaki klabuni humo.

Mshambuliaji wa Everton raia wa Norway Josh King anafanya mazungumzo na Galatasaray ya Uturuki na mchezaji huyo wa miaka 29 anaonekana kuwa na nia ya kuondoka klabu hiyo msimu huu wa joto.

Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, anatamani kurudi Manchester United msimu huu wa joto.

 

Ronaldo Yupo Tayari Kurejea United na Kupunguzwa Mshahara?

Arsenal wana wasiwasi kuwa wanaweza kumpoteza mchezaji kutoka Norway Martin Odegaard, 22, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Real Madrid, kwa sababu ya kujitoa kwenye Ligi Kuu ya Ulaya.

Liverpool wamekubaliana masharti ya kibinafsi na RB Leipzig kwa beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 21, ambaye kifungu cha kuachiliwa kwake kutoka kwa klabu hiyo ya Bundesliga ni £ 34m.

Tetesi zinasema Kocha wa muda wa Sheffield United Paul Heckingbottom anatarajia kiungo wa kati wa Norway 23 Sander Berge kubaki na klabu hiyo iliyoshuka daraja, licha ya nia kutoka kwa Arsenal na Tottenham kumsajili.

Tetesi zinasema Barcelona wanajaribu kumrudisha tena kiungo wa Ufaransa Kays Ruiz-Atil klabuni huku mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 18 huko Paris St-Germain ukimalizika mwishoni mwa msimu.

Mlinda lango chaguo la tatu wa Manchester United Lee Grant, mwenye umri wa miaka 38, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo msimu huu wa joto na Muingereza huyo akihisi kuwa klabu hiyo imekiuka makubaliano ya kumpa mktaba mpya

Meneja wa Brighton Graham Potter anasema kiungo wa Mali Yves Bissouma anaweza kuimarika na the Seagulls, ambao hawapaswi kuogopa nia ya timu nyingine zinazotaka huduma zake kama vile Liverpool.

Tetesi zinasema Afisa mkuu Mtendaji wa Manchester United anayemaliza muda wake Ed Woodward anatarajiwa kuchagua mrithi wake kabla ya kuondoka klabuni hapo.

 

manchester united ed woodward

Newcastle itahitaji kuilipa Arsenal takribani pauni milioni 20 ili kumsajili kiungo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 Joe Willock kwa mkataba wa kudumu.

Tetesi zinasema Mmiliki wa Leeds Andrea Radrizzani anatumai meneja Marcelo Bielsa ataongeza kandarasi yake huko Elland Road kabla ya mwisho wa msimu huu.

Kiungo wa kati wa Aston Villa, Carney Chukwuemeka, 17, anafuatwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia ikiwamo Manchester United na Manchester City.

Mlinzi wa Manchester City mreno Pedro Porro, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Sporting Lisbon, anaivutia Real Madrid inayomezea mate huduma zake.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa