Tetesi zinasema, Chelsea wanaongoza mbele ya Manchester United na Paris St-Germain katika mbio za kumsajili beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane, 28.

Beki wa Guinea Ali Camara, 23, ambaye anachezea klabu ya Young Boys ya Switzerland, amezivutia klabu kadhaa za Ligi ya Primia zikiwemo Liverpool, Arsenal, Crystal Palace, West Ham United na Norwich.

Tetesi zinasema, Kalbu ya Bayern Munich imeanzisha mazungumzo ya kutaka kumsajili kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann.

Arsenal wapo njia panda juu ya mustakabali wa kiungo wao Joe Willock, 21, ambaye yupo Newcastle kwa mkopo. Klabu hiyo wanahitaji kuuza baadhi ya wachezaji ili kujiimarisha kifedha.

Tetesi zinasema Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ana nia ya kumsajili beki raia wa Uhispania Cesar Azpilicueta, 31, kutoka katika klabu ya Chelsea.

Manchester United na Liverpool wanaweza kujaribu kumsajili msahambuliaji wa Torino na raia wa Italia Andrea Belotti, 27, pia anazivutia AC Milan, Roma na Inter.

Wolverhampton Wanderers imeingia katika orodha ya klabu ambazo zinapigiwa upatu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Tammy Abraham, 23. Aston Villa, West Ham na Leicester City pia wanadaiwa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.

Kocha wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anategemea kuwa mshambuliaji Harry Kane, 27, kuendelea kusalia katika klabu hiyo licha ya tetesi kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema Manchester City wameanza majadiliano na Red Star Belgrade kwa nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Serbia Andrija Radulovic, 18.


Kwani Meridianbet Wanasemaje! Mkwanja Upo Kwenye Kasino mpya ya Mini Power Roulette.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa