Tetesi zinasema, Manchester United bado wanataka kufanya usajili wa winga wa kulia mwishoni mwa msimu, huku mchezaji nyota wa timu ya taifa ya England na klabu ya Borussia Dortmund, Jadon Sancho, 21, akiendelea kuwa kipaumbele.

Tetesi zinasema, Chelsea watapokea ofa za kuanzia pauni milioni 40 kwa klabu zitakazotaka kumsajili mshambuliaji wake Tammy Abraham, 23, mwishoni mwa msimu.

Vigogo hao wa London maarufu kama the Blues wanaandaa kitita cha pauni milioni 90 ili kumrejesha klabuni hapo mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, 27.

 

Lukaku Inter

Tetesi zinasema, Everton wanataka kumsajili beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral, 23.

Arsenal pia wanajiandaa kumuuza beki wao wa pembeni Hector Bellerin, 26, na kuchukua nafasi yake wanataka kumsajili beki wa Norwich Max Aarons, 21.

Beki wa kati wa Chelsea Fikayo Tomori, 23, amekutana na mkurugenzi wa klabu ya AC Milan Paolo Maldini. Milan wanataka kumsajili moja kwa moja mchezaji huyo ambaye sasa anaichezea klabu hiyo kwa mkopo.

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 34, hatarajiwi kuongeza mkataba na klabu yake ya Chelsea.

 

Inter Yaingia Mazima kwa Giroud.

Arsenal wanakusudia kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Mjerumani Julian Brandt, 24. Usajili huo unaweza ukawa ni wa kuziba pengo la Martin Odegaard endapo kama Real Madrid watamtaka mchezaji wao huyo kurejea kikosini mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema, Beki wa klabu ya Sevilla Jules Kounde, 22, ambaye alikuwa awali ananyemelewa na Chelsea sasa anawindwa na Real Madrid.

Tetesi zinasema, Burnley wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 9 kumsajili beki Nathan Collins, 19, kutoka Stoke City.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa