Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Atletico Madrid msimu uliopita amemtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kusalia Nou Camp.

Tetesi zinasema, Aston Villa ipo kwenye tahadhari baada ya kujitokeza kuwa Chelsea iko tayari kukubali ofa ya takriban pauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji Tammy Abraham, 23.

Borussia Dortmund imeingia kwenye kinyanganyiro cha kumsajili mlinzi wa Uingereza Ben White, 23, huku Paris St-Germain, Manchester United na Arsenal zikimnyatia mchezaji huyo.

 

Dortmund, United na Arsenal kwa Ben White

Inter Milan inafikiria kutoa ofa yake ya mkataba mpya kwa mlinzi wa England Ashley Young, 35 ikiwa itashinda kombe la Serie A wikendi hii. Watford pia inataka kumsajili.

Tetesi zinasema, Everton ni miongoni mwa vilabu kadhaa za Ligi ya Primia zinazo msaka mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 25.

Kiungo wa kati wa Arsenal Bukayo Saka, 19, amesema hakusita kutia saini makubaliano mapya na Gunners, licha ya Borussia Dortmund na Liverpool kuonesha kuwa nazo zinamtaka.

West Ham na Newcastle zimeonesha nia ya kumsajili Mario Lemina wa Southampton. Kiungo huyo wa kati raia wa Gabon, 27, sasa hivi yuko Fulham kwa mkopo na anapatika kwa kima cha pauni milioni 7.

 

Christensen Anatumaini la Kuongeza Mkataba Darajani

Mlinzi wa Chelsea, Andreas Christensen, 25 amesema anataka kutia saini makubaliano mapya na klabu hiyo licha ya kudumu Stamford Bridge kwa miaka 10 sasa.

Tetesi zinasema Leeds imekataa ofa kutoka kwa Legia Warsaw ya kumchukua mchezaji wa Poland Mateusz Bogusz, 19, msimu ujao kwa mkopo.

Southampton inamfuatilia mlinda lango wa West Brom Josh Griffiths kabla ya uwezekano wa kumsajili kipindi cha uhamisho mchezaji huyo, 19, ambaye ameonesha umahiri wake Cheltenham akiwa huko kwa mkopo msimu huu.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa