Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Mei 6,2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Liverpool wamekubaliana kuhusu masharti binafsi na kiungo wa kati wa Ufaransa na RB Leipzig Ibrahima Konate, 21, anayejiandaa kujiunga na klabu ya primia kwa mkataba wa miaka mitano. 

Tetesi zinasema, West Ham imejiunga na Chelsea na vilabu vingine katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 25, ambaye ana gharama ya pauni milioni 35.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah anataka kuondoka Liverpool na Paris St-Germain wanapanga kumpata mchezaji huyo ,28, ikiwa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe,22, ataondoka majira ya joto.

Wakati huo huo, PSG wanatafuta kuimarisha safu ya ulinzi na wamebainisha kuwa mlinzi wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier,28, kuwa ni lengo lao muhimu.

Tetesi zinasema, Norwich City wako kwenye mchuano na Southampton na West Ham kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi kinda Brandon Williams,20, kwa mkopo anayekipiga Manchester United.
Tetesi za soka- baleTetesi zinasema, Tottenham imefanya mazungumzo na kocha wa Inter Milan Antonio Conte kuhusu nafasi iliyo wazi ndani ya Spurs. Mazungumzo na Muitaliano huyo, 51 yamekuja baada ya Conte kuiwezesha Inter kutwaa taji lao la kwanza baada ya miaka 11. 

Tetesi zinasema, Jose Mourinho anaweza kumtaka nahodha wa zamani Daniele De Rossi,37, kuungana naye kama kocha msaidizi atakapochukua nafasi ya kocha wa AS Roma msimu ujao.

Tetesi za soka.Tetesi zinasema, Kocha wa zamani wa Spurs Mourinho atatazama uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Erik Lamela,29, na mshambuliaji wa Brazil Lucas Moura,28.

Tetesi zinasema, Vinginevyo, Mourinho atatafuta wachezaji wawili wa Spurs Muingereza Eric Dier, 27, na Dane Pierre-Emile Hojbjerg, 25, pamoja na mchezaji wa Uhispania wa Manchester United Juan Mata, 33.

Tetesi zinasema, Uimara wa mshambuliaji wa Brazil Wesley,24, ambaye hivi karibuni alirejea baada ya kuwa benchi kwa karibu miezi 16 kutokana na jeraha kubwa la mguu, kutategemea kama Aston Villa watamsajili mshambuliaji mwingine.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya, Meridianbet

SOMA ZAIDI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa