Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Mei 18, 2021 zinasema:-

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa England Harry Kane kwa mara nyengine ameambia Tottenham anataka kuondoka katika klabu hiyo ya ligi ya England mwisho wa msimu huu. Manchester City, Chelsea na Man United zimeonesha hamu ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Manchester United itashindana na Manchester City katika ununuzi wa beki kinda wa Sporting Lizborn Nuno Mendes kwa dau la £52m.

Leeds United na mabingwa wa Uskochi Rangers wanamchunguza mchezaji wa klabu ya America de Cali mwenye umri wa miaka 21 raia wa Colombia Santiago Moreno.

Tetesi za soka - Kane

Tetesi zinasema, Mchezaji wa England Kieran Trippier amehusishwa na hatua ya kurudi katika ligi ya England , huku Manchester United na Everton zote zikishindana kupata saini ya beki huyo wa kulia kutoka Atletico Madrid..

Klabu ya Brighton & Hove Albion imeambia Liverpool na Arsenal itachukua dau la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Mali mwenye umri wa miaka 24 Yves Bissouma.

Manchester United inaiongoza Ajax katika mbio za kumsaini mshambuliaji wa Ghana Kamaldeen Sulemana kutoka FC Nordsjaelland baada ya mazungumzo ya kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 siku ya Jumatatu..

Beki wa Uhispania Marcos Alonso, 30, na beki wa kushoto wa Itali mwenye umri wa miaka 26 Emerson Palmieri wanapigania kuondoka Chelsea mwisho wa msimu huu ili kujaribu kutafuta fursa katika ligi ya Serie A , kwa kuwa wote wanataka kuhisi kwamba wao ni muhimu kwa mara nyengine.

Tetesi za soka - Kieran TrippierBeki wa Uholanzi Patrick van Aanholt, 30, anatarajiwa kuondoka Crystal Palace wakati kandarasi yake itakapokamilika

Mshambuliaji wa klabu ya Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 27, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Barcelona kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu.

Mchezaji wa Ivory Coast na aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Gervinho, 33, anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Itali ya Serie A Parma mwisho wa kandarasi yake ili kujiunga na klabu ya Uturuki ya Trabzonspor.


Unaweza kuwa milionea wakati wowote!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya, MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa