Tetesi zinasema Chelsea imewasiliana na Bayern Munich kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski , lakini klabu hiyo ya ligi ya Premia inakabiliwa na changamoto kuu ya ushindani kutoka kwa Paris St Germain na Barcelona.

Mshambuliaji wa England Harry Kane anataka kuhamia katika klabu ya Manchester City kwa dau la £100m mwisho wa msimu huu . Manchester United inamfwatilia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 licha ya kwamba Spurs haiko tayari kumuuza kwa wapinzani wao wa jadi mjini London Chelsea.

Tetesi zinasema Tottenham ilianza mipango ya kumuuza Kane mwezi Februari na kuonesha uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema Crystal Palace ipo katika mazungumzo na aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea na kiungo wa kati wa England Frank Lampard, 42, kuhusu kumrithi Roy Hodgson.

Aliyekuwa mkufunzi wa Bounemouth Eddie Howe, 43, pia yupo katika orodha ya kumrithi Hodgson mwenye umri wa miaka 73 , huku mkufunzi wa Swansea mwenye umri wa miaka 42 Steve Cooper na kocha wa Barnsley Valerien Ismael 45 pia wakionekana kuwa kifua mbele kuchukua mahala pake.

Tetesi zinasema winga wa Arsenal na Brazil mwenye umri wa miaka 32 Willian anataka kuondoka ili kujiunga na klabu ya David Beckham Inter Miami Marekani.

Tetesi zinasema Barcelona inaweza kumwachilia kipa wa Brazil Neto kuondoka mwisho wa msimu huu , huku Arsenal ikiwa na hamu kuendelea kusaka saini ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 31.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema Southampton inapanga kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Denmark na Borussia Dortmund Thomas Delaney, 29.

Tottenham imewasilisha ombi la beki wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Matthias Ginter lakini inakabiliwa ushindani kutoka kwa Liverpool na Inter Milan kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Tetesi zinasema Aston Villa imewasiliana na wawakilishi wa winga wa Algeria Bordeaux’s Mehdi Zerkane, 21, baada ya kumchunguza mchezaji huyo kwa miezi kadhaa.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa