Tetesi zinasema Manchester United huenda ikawasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Southampton na England Danny Ings ,28 , mwisho wa msimu ili kuimarisha safu ya mashambulizi ya mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer.

Chelsea imewasilisha ombi la dau la £80m kumnunua mshambuliaji wa England na Borrusia Dortmund Jadon Sancho , lakini klabu hiyo ya London inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Man United.

Tetesi zinasema, klabu barani Ulaya ikiwemo Tottenham ,Chelsea, Borussia Dortmund na AC Milan zinatarajiwa kushindana kumsaini kipa wa England Dean Henderson, kutoka Man united.

 

Henderson

Kiungo wa kati wa Juventus na Wales Aaron Ramsey ameivutia klabu ya Liverpool kulingana na ripoti nchini Itali . The Reds wamesemekana kufikiria kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal katika dirisha lijalo la uhamisho.

Tetesi zinasema Chelsea imehusishwa na ununuzi wa kiungo wa kati wa Ufaransa na Monaco 21.

Mkufunzi wa Bayern anayeondoka Hansi Flick, 56, ambaye amehusishwa na kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani , anatakiwa na Barcelona kama mkufunzi atakayechukua mahala pake mkufunzi aliyepo sasa Ronald Koeman .

Tetesi zinasema, Barcelona iko tayari kusikiliza ofa za mshindi wa kombe la dunia Mfaransa Antoine Griezman ili kupunguza mzigo wa kifedha wa klabu hiyo.

Griezmann, 30, huenda akarudi katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid katika makubaliano ambayo huenda yakampatia fursa Joao Felix kuelekea Barcelona , japokuwa klabu hiyo ya Catalan haijakubali ofa hiyo.

 

Griezmann: Sipo Katika Ubora Wangu.

Klabu ya Jose Mourinho , Roma ipo katika nafasi nzuri ya kumsaini mshambuliaji wa Itali na Torino Andrea Belotti. AC Milan pia wapo mbioni kutaka kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 , lakini pia wanamlenga mashambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho mwa msimu huu.

Everton na Arsenal wanamchunguza beki wa Real Betis Emerson Royal. Mchezaji huyo wa Brazil , 22, yupo kwa mkopo kutoka Barcelona lakini huenda akavutiwa kucheza katika ligi ya Premia iwapo hatochezeshwa mara kwa mara katika uwanja wa Nou.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., MeridianbetBASHIRI SASA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa