Tetesi zinasema, klabu ya Leicester City imepanga kumsajili kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho (29), ingawa bado haijapeleka ofa rasmi, klabu hiyo iko kwenye mazugumzo ya kumnasa Mbrazili huyo ikiwezekana kwa ada ya £17m au kwa mkopo.

Klabu ya Leeds United inamtaka beki wa kushoto wa Lyon, Maxwel Cornet, (24) lakini dau walilotajiwa la £20m kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, linawafanya kusita.

Tetesi zinasema, Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti amewaarifu mabosi wa klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, mjerumani Timo Werner (25).

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Kiungo wa kihispania, Juan Mata, 33, atalazimika kuchukua mshahara kiduchu wa £70,000 kwa wiki kama anataka kuendelea kusalia Manchester United baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Tetesi zinasema, Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta yuko tayari kumuuza mlinda mlango, raia wa Ujerumani Bernd Leno (29), msimu huu kama atapatikana mbadala wake.

Chelsea imeongeza dau kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa Inter Milan, raia wa Morocco Achraf Hakimi, ikiwemo kitita taslimu cha £43m pamoja na kumtoa nyota wa kimataifa wa Italia Emerson Palmieri (26).

Mwenyekiti wa Klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema atafanya kile kilicho sahihi kwa klabu kuhusu masuala ya usajili, ikiwemo mustakabali wa mshambuliaji Harry Kane, aliyeonyesha nia ya kutimka msimu huu.

 

Tottenham : Kane Sokoni, Halland White Hart Lane.
Harry Kane

Liverpool inaongoza mbio za kuwania saini ya beki wa Juventus, Cristian Romero raia wa Argentina, ambaye awali alihusishwa na mipango ya kumtimkia Manchester United, baada ya kuonyesha kiwango kizuri akichezea Atalanta kwa mkopo.

Mlinda mlango wa Hispania David de Gea, 30, inaelezwa kwamba hajui hatma yake ndani ya Manchester United wakati huu akijiandaa kufanya mazungumzo.

Southampton na West Ham ni vilabu vya hivi karibuni kutoka ligi kuu ya England kuhusishwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Boavista Alberth Elis (25), huku vilabu vya Brighton na Watford awali vilionyesha pia nia yao ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Honduras.

Klabu ya Borussia Dortmund itatumia kipengele maalumu kuhuisha mkataba wa Jude Bellingham atakapotimiza miaka 18 baadae mwezi huu, ili kiungo huyo wa England asalie katika klabu hiyo ya Bundesliga mpaka mwaka 2025.

Arsenal wanamuwania kiungo mfaransa, Nabil Fekir kutoka Real Betis, lakini ofa ya washika bunduki hao haifikii kiwango wanachohitaji klabu hiyo ya La Liga kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.

Crystal Palace inajiandaa kupeleka ofa ya £15 kwa ajili ya kiungo wa kiingereza Conor Gallagher (21) kutoka Chelsea, ambaye anataka kusalia Stamford Bridge baada ya msimu uliopita kuonyesha kiwango kizuri akiwa West Brom kwa mkopo.

Kiungo wa England, Jesse Lingard, 28, ameimwmabia meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kwamba anataka kusalia kwa mashetani hao wekundu, baada ya kuwa na wakati mzuri msimu uliopita aikiwa na West Ham kwa mkopo.

Tetesi zinasema, Mlinda mlango wa Juventus, aliyenyakuwa pia kombe la dunia akiwa na Italia, Gianluigi Buffon, 43, anajiandaa kurejea Parma, ya Serea B, ikiwa ni miaka 20 tangu aondoke kwenye klabu hiyo.

 

Buffon Atastaafu Soka au Kurejea Barcelona?

 

Tetesi zinasema, kiungo wa Tottenham, mfaransa Moussa Sissoko (31) anawaniwa na klabu ya Napoli inayoshiriki ligi kuu ya Italia, Serie A.

Meneja wa Norwich City Daniel Farke anataka kumsajili kiungo wa Bournemouth raia wa Denmark, Philip Billing (25), ambaye anataka kuondoka baada ya kabu hiyo kushindwa kupanda daraja kucheza ligi kuu ya England.

Tetesi zinasema, Kiungo wa Bernardo Silva (26) anataka kutimka Manchester City, huku vilabu vya Barcelona na Atletico Madrid vikionyesha nia ya kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Ureno.

Tetesi zinasema, Leeds United inahusishwa na mpango wa kumsajili mlinzi wa kushoto wa Rangers, raia wa Croatia Borna Barisic (28).

Mlinzi wa Juventus, raia wa Romania, Radu Dragusin anawaniwa na klabu ya Crystal Palace, ambayo tayari imeshapeleka ofa kwa ajili ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa