Tetesi zinasema, Manchester City wako tayari kumtoa mmoja wa wachezaji nyota akiwemo mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 24, nahodha wa Algeria Riyad Mahrez, 30, kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 26, au mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 26, kama sehemu ya mpango wa kuishawishi Tottenham kuwauzia nahodha wa Uingereza, Harry Kane.

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, hatakubali mkataba mpya Paris St-Germain kwani anajiandaa kuhamia Real Madrid, licha ya klabu hiyo ya Ufaransa kutaka kumuunganisha na mchezaji mwenzake wa kimataifa Paul Pogba.

Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu wa joto baada ya kukataa mkataba wa pauni milioni 350 kwa wiki licha ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Premia kutaka akamilishe mkataba wake wa sasa na kuondoka 2022.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Manchester United pia wanang’ang’ana kufikia makubaliana na Real Madrid kumsajili beki wa Ufaransa Raphael Varane, 28. Klabu hiyo ya La Liga inataka kulipwa £50m kumuachilia mlinzi huyo huku United wakiwa tayari kulipa £40m.

Tetesi zinasema, Liverpool ni miongoni mwa klabu kadhaa za Ulaya zinazotafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na timu ya taifa ya Ivory Coast Franck Kessie, 24.

Newcastle wana imani ya kumpata kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 27, baada ya kufanya mazungumzo na wachezaji kadhaa wa safu ya kati ambao bei yao iko nje ya viwango vya mshahara wa klabu hiyo.

Tetesi zinasema, Eden Hazard, 30, tayari ameonesha wazi hisia zake kwamba kurejea kwake Chelsea haina mjadala baada ya vyombo vya habari vya Uhispania kuripoti kuwa Real Madrid inatafuta njia ya kumuuza.

 

Eden Hazard

Tetesi zinasema, Arsenal imeambiwa na Sheffield United kuongeza ofa ya kumnunua Aaron Ramsdale ,32, kwa hadi pauni milioni 32 baada ya kukataa mara mbili dau la kumuuza kipa huyo.

Tetesi zinasema, Chelsea wanamfwatilia Sergio Romero, 34, baada ya mkataba wake na Manchester United kukamilika.

Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Roma baada ya klabu hiyo ya Serie A kumaliza pre season.

Tetesi zinasema, Aston Villa huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Argentina Julian Alvarez wiki ijayo.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

  1. Uhamisho wa Harry Kane kwenda City kunataka kuibomoa Mancity kabisa, City wanatakiwa kuwa Makini katika kukamilisha mchakato huu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa