Tetesi zinasema, Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na Real Madrid kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 28, kwa dau la £42m.

United pia wanaweza kumsajili kiungo wa hispania Saul Niguez kutoka kwa mabingwa wa La Liga Atletico Madrid kwa dau la £45m. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa pia na vilabu vya Barcelona na Juventus.

Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili nyota anayewaniwa na Liverpool Donyell Malen, 22 kwa dau la £26m.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet
Donyell Malen 

Winga wa Argentina Erik Lamela, 29, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Tottenham kwenda Sevilla, huku Winga wa Hispania Bryan Gil, 20, akielekea upande wa pili.

Tetesi zinasema, Newcastle watamgeukia kiungo wa Chelsea na England Ross Barkley, 27, iwapo watashindwa kumsajili Joe Willock, 21, kutoka Arsenal.

Juventus imepanga kufanya mazungumzo mengine mapya na Sassuolo wakipambana kumshawishi kungo wa Italia Manuel Locatelli anayewaniwa pia na klabu ya Arsenal.

 

Sassuolo Wathibitisha Kupokea Ofa ya Locatelli Toka Arsenal

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wamefanya mazungumzo na wakala wa Kalidou Koulibaly katika harakati zao za kumsajili mlinzi huyo wa Napoli and Senegal mwenye umri wa miaka 30.

Tetesi zinasema, Kiungo wa Uhispania Isco, 29, hatapewa mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid. Mkataba wake wa sasa unamalizika msimu ujao.

Kiungo wa Chelsea na Scotland Billy Gilmour, 20, ameonyesha kipaji chake cha sauti kwa kuimba karaoke classic katika mgahawa mmoja huko Norwich, ambapo yupo huko kwa mkopo.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer anataka kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 28, kusalia katika klabu hiyo, huku Paris St-Germain ikimtaka.

Arsenal, Tottenham na Everton wanangalia uwezekano wa kumchukua kiungo wa safu ya ushambulizi Muargentina Joaquin Correa, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka Lazio msimu huu.

Juventus wamekataa dau la pauni milioni 86 kutoka kwa Liverpool kwa ajili ya Federico Chiesa. Winga huyo mwenye umri wa miaka 23,alikuwa mchezaji nyota wa Italia katika Euro 2020.


KUWA SHUJAA KATIKA KASINO ZA MERIDIANBET!

SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa