Tetesi zinasema, Manchester City wako tayari kulipa pauni milioni 130 kwa ajili ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, na wamesalia kuwa na matumaini kwamba wanaweza kusaini mkataba naye.

Tetesi zinasema, Arsenal wamependekeza mkataba wa nyongeza ya pesa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison. The Gunners wanasita kulipa pauni milioni 60.

Inter Milan watakubali kwa shingo upande dau la takriban pauni milioni 100 kutoka kwa mshambuliaji wa Chelsea Mbelgiji Romelu Lukaku, 28, baada ya maafisa katika klabu hiyo kukubali kibinafsi kuwa wanahitaji kumtoa mmoja wa wachezaji mashuhuri msimu huu ili kuweka sawa mahesabu yao ya pesa.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Mlinzi wa Uhispania Aymeric Laporte ameieleza wazi Manchester City kwamba anahitaji kuhamia La Liga msimu huu, huku Barcelona na Real Madrid zikiwa makini kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Tetesi zinasema, Southampton na West Ham zinamtaka mlinzi wa kikosi cha vijana wenye umri wa miaka 21 wa Nice na Austria-21 Flavius Daniliuc, 20.

Liverpool, pamoja na timu zisizojulikana za Primia ligi, wanataka kusaini mkataba na mshambuliajii wa Bournemouth Mholanzi Arnaut Danjuma, 24, ambaye tayari anatakiwa kwa dau na timu ya Villarreal. The Cherries wanasemekana kumtaka kwa mkataba huru wa pauni milioni 21.5.

Aston Villa wana matumaini ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, na mlinzi wa Manchester United Axel Tuanzebe, 23.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Chelsea wamemtoa kama ofa winga Mbrazili Kenedy kwa klabu ya Sevilla ikiwa ni kama sehemu ya mkataba wao na Jules Kounde,22, baada ya mlinzi mwenzake Mfaransa Kurt Zouma, 26, kutolewa awali katika sehemu ya kubadilishana wachezaji na the Blues.

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo atataka bado kuondoka Juventus kuelekea Real Madrid, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, anafahamu kuwa fursa zake za kurejea Bernabeu zinategemea iwapo klabu hiyo ya Uhispania itafanikiwa katika harakati zake za kumtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain, 22 Mfaransa Kylian Mbappe.

Tetesi zinasema, Brentford wanakamilisha mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati wa Midtjylland Msweden Swedenn 21, Jens Cajuste, ambaye amehusishwa na taarifa za kuhamia katika klabu ya Rennes.

 

Zlatan Ibrahimovic

Tetesi zinasema, Mshambuliaji Msweden Zlatan Ibrahimovic, 39, alitaka kurejea Paris St-Germain kabla ya kukubali mkataba mpya wa mwaka mmoja katika AC Milan.

Leeds United wana ushindani katika dau la kusaini mkataba na mchezaji wa kikosi cha vijana walio china ya umri wa miaka 21 cha Uholanzi Noa Lang. Kulingana na ripoti klabu ya ligi ya Uhispania Sevilla pia wanamtaka winga huyo mwenye umri wa miaka 22.

Tetesi zinasema, West Brom wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji wa klabu ya Derby County kutoka Wales Tom Lawrence mwenye umri wa miaka 27.


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa